July 22, 2018


Na George Mganga

Kocha wa makipa, Mussa Mbaya, maarufu kwa jina la Moloto, amerejea tena Kagera Sugar kwa kusaini kandarasi ya miaka miwili.


Moloto amefikia makubaliano na uongozi huo wa wakata miwa kwa kukubaliana dili hilo akitokea Ndanda FC ya Mtwara baada ya kuitumikia klabu hiyo kwa msimu mzima wa 2017/18.


Kocha Moloto kabla ya kwenda Ndanda alikuwa akiinoa Kagera Sugar msimu wa 2016/17 na baada ya hapo akaelekea zake Mtwara kuungana na walima korosho hao.


Kocha huyo mwenye kipaji maridadi cha kufundisha makipa na wachezaji wa ndani na akiwa na leseni ya Ukocha wa Makipa kutoka FIFA, ameahidi kuutendea haki mkataba wake na Kagera ili kuhakikisha malengo yake yanatimia msimu ujao wa Ligi Kuu Bara.


Mbali na kutendea haki mkataba huo, Moloto ameandaa kliniki maalum ya kufundisha wachezaji vijana wenye fani ya ugolikipa itakayokuwa inafanyika ndani mkoani Kagera katika Manispaa ya Bukoba mara moja kila mwisho wa mwezi.


Moloto ameamua kuandaa kliniki hiyo kwa lengo la kuibua na kukuza vipaji vya vijana ili baadaye waweze kuwa sehemu ya taifa la kesho na ikiwezekana kuleta maendeleo kisoka kupitia timu ya taifa.



0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic