July 22, 2018





Ile historia ya Simba kutoa ruhusa kwa wachezaji wake kila wanapopata nafasi kucheza nje ya Tanzania, imeendelea kujirudia.

Maana beki wa mabingwa hao wa Soka Tanzania, Simba, Juuko Murshid ameanza kufanya majaribio katika klabu ya Super Sport United ya Afrika Kusini.


Juuko ameanza majaribio kwa ruhusa kutoka uongozi wa Simba ambao ulimuachia ili ajaribu bahati yake.

Kaimu Rais wa Simba, Salim Abdallah ’Try Again’, amethibitisha uongozi wake kumuachia Juuko kwenda Afrika Kusini.

“Anaendelea vizuri huko Afrika Kusini, uongozi ulimpa nafasi ya kujaribu. Kama atafanikiwa basi tutaingia katika mazungumzo,” alisema.

Simba imekuwa na utamaduni wa kuwapa nafasi wachezaji wake ambao wamepata ofa katika nchi mbalimbali.

Juuko ambaye anakipiga timu ya taifa ya Uganda, The Cranes amekuwa pia akiwaniwa na timu nyingine ya Afrika Kusini ya Bidvest.

Tayari kikosi cha Simba kipo nchini Uturuki kwa ajili ya kambi ya wiki mbili kujiandaa na msimu mpya wa Ligi Kuu Tanzania Bara.

3 COMMENTS:

  1. Hii ndio timu ambayo inataka kushindana na timu nyingine Afrika kama TP Mazembe lakini umewahi kusikia mazembe inauza wachezaji wake kwa timu nyingine afrika kwa kifupi simba ni kama imepata mfadhili ila siyo mwekezaji makini ndio maana mpaka sasa hakuna mipango yoyote ya ujenzi wa kiwanja wala kukarabati ofisi za simba kwani jengo lao limepitwa na wakati

    ReplyDelete
  2. Huyu Dewji ni Mfadhili tu! Maneno mengi hatuoni uuzaji wa hisa wala nini!Hawa watafika mahala watakwama tu.

    ReplyDelete
    Replies
    1. Kama kstiba bado aijapita kwa msajili unategemea mo atafanyanini muemnafikiria kwani akunamtu mwenyeuwezo wakuvunja sheria za nnchi

      Delete

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic