July 23, 2018


Baada ya kukutana na viongozi wa juu, hatimaye wachezaji wa klabu ya Yanga wameridhia kuanza mazoezi leo kujiandaa na mchezo wa Kombe la Shirikisho Afrika dhidi ya Gor Mahia.

Yanga iliitisha kikao Maalum kupitia uongozi wake kikiongozwa na Kaimu Mwenyekiti, Clement Sanga pamoja na Mwenyekiti wa Kamati ya Usajili, Hussein Nyika kunako makao makuu ya klabu hiyo ili kutatua mgomo wa wachezaji wa timu yao.

Ikumbukwe mapema baada ya kikosi cha timu hiyo kurejea nchini baada ya kichapo cha mabao 4-0 dhidi ya Gor Mahia kwenye mchezo wa mkondo wa kwanza, wachezaji wake waligoma kuendelea na program ya mazoezi kwa madai ya kutolipwa fedha zao.

Kutokana na tukio hilo la kugomea mazoezi limewafanya viongozi wa Yanga kukutana jana na wachezaji wao ili kulizungumzia na mwafaka umefikia ambapo leo wataanza tena mazoezi kwenye Uwanja wa Chuo cha Polisi, Kurasini.

Yanga itakuwa kibaruani Jumapili ya wiki ijayo kucheza dhidi ya Gor Mahia katika mchezo wa kundi D utakaokuwa wa mkondo wa pili Julai 29 kwenye Uwanja wa Taifa, Dar Es Salaam.

4 COMMENTS:

  1. Kwa ubavu gani iliyonayo Yanga wa kutoa dozi kwa Gor Mahia?mwandishi acha masihara

    ReplyDelete
  2. Ebu rudia comment uliyoiandika km inaleta maana uliyoikusudi?

    ReplyDelete
  3. Dozi la kuwamaliza Gor Maria? au umesahau mlifungwa 4G. Hebu eleza ukweli Yanga watawamaliza vipi Gor.Hawafanyi mazoezi..Wana miesi mitatu hawajalipwa.

    ReplyDelete
    Replies
    1. mwandishi achana na ndoto za mchana.na sio vizuri kuandika mzaha

      Delete

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic