Laudit Mavugo ambaye msimu uliopita aliichezea Simba, amepata taarifa kuwa timu hiyo imemsajili Meddie Kagere hivyo kwa hali ilivyo ni vyema John Bocco akaanzia benchi na kuwapisha Kagere na Emmanuel Okwi kikosi cha kwanza.
Mavugo ambaye msimu uliopita aliifungia Simba mabao manne kwenye ligi, alisema anamfahamu sana Kagere na aliwahi kucheza naye katika klabu ya Polisi Rwanda hivyo hakuna mtu wa kumdanganya kuhusu uwezo wake.
“Nimesikia Kagere amesaini Simba, kwangu ni mchezaji mzuri ambaye anajua kufunga kwa sababu nilishawahi kucheza naye kwenye timu moja ya Polisi Rwanda na alikuwa anafunga sana, nadhani atakuwa msaada mkubwa kwao katika michuano ya kimataifa.
“Binafsi naona ni vizuri kocha akamuanzisha pamoja na Okwi kwa kuwa wote ni wafungaji wazuri, siyo kwamba Bocco hawezi, hapana ila naona kama Bocco akitokea benchi itakuwa vizuri kwao lakini Kagere aanze na Okwi halafu waone kitakachotokea,” alisema Mavugo ambaye ni mchezaji kipenzi wa Haji Manara anayemuita King Mavugo.
Mavugo ameondoka Smba baada ya kumaliza mkataba wake na timu hiyo mapema baada ya msimu wa 2017/18 kumalizika.








Kagere si utani jamaa mwingi wa mengi si mchezo. Kitu kimoja Watanzania sisi ni watu kuchonga sana tena cha kushangaza zaidi ni pale unapoona mtu akitapika maneno yake ya hovyo kwenye vyombo vya habari kwa maandishi,ooh Meddie Kagere ni mzee kabisa wala miaka 32 sio yake? Kama vile ana stakabadhi zote na ushahidi mkononi juu ya umri wa Kagere. Kama kagere au watu wake wa karibu kama vile wakala wake, wakiamua kuburura mahakamani ukathbitishe utasemaje?
ReplyDeleteHakuishia hapo tu akaendelea kuthibitisha kusema hata Okwi sio umri wake kwani hawezi kuwa mdogo kuliko John Boko? Sisi Watanzania hatuna tabia ya kuwabagua wageni au kuwasimanga hii kasumba inatokea wapi? SIMBA walipomleta Okwi kutoka Uganda alikuwa kijana mdogo sana miaka 16 au 17 yaani simba walianza na kazi ya kulea kwanza kwa Okwi kabla ya kuanza kuisadia timu na ndio maana Okwi simba sio kazini ni nyumbani kabisa. Kuna wachezaji wana miaka mpaka 47 kwa wenzetu bado na wanacheza soka la ushindani na husikii kuitwa wazee na hata akiitwa mzee ni kwa heshima sio kwa kejeli. Kama mtu anatafuta point ya kutengeneza hoja yake muache afanye hivyo lakini sio kwa kuwakashifu watu wengine bila yakuwa na uhakika na anachokisema.
(h)
ReplyDelete