MKALI wa Singeli, Man Fongo leo ameondoka na kijiji chake alipopanda jukwaani na kupiga nyimbo zake zote kali katika Tamasha ba’b kubwa la Tusua Maisha lililoandaliwa na Global Publishers kwa ajili ya kuwashukuru wasomaji wake wa magazeti ya Risasi, Championi, Uwazi, Ijumaa, Amani na Spoti Xtra.
Man Fongo ambaye pia anatamba na Wimbo wa Hainaga Ushemejji alianza kusepa na kijiji alipoingia na kupiga nyimbo zake zote kali kuanzia Kujinafasi, Sio Poa na kionjo cha Hainaga Ushemeji.
Katika tamasha hilo ambalo washindi wanne walipata bahati ya kupata simu za mkononi baada ya kujaza kuponi za gazeti la Spoti Xtra na kisha droo fupi kuchezeshwa.
0 COMMENTS:
Post a Comment