July 10, 2018


Beki wa zamani wa Real Madrid Michel Salgado anaamini mshambuliaji wa Tottenham na Uingereza Harry Kane, 24, ndiye anayelengwa na klabu hiyo msimu huu baada ya mshambuliaji wa Paris St-Germain na Brazil Neymar, 26. (Talksport)

Chelsea inajaribu kuipiku Manchester City katika kumsaini kiungo wa kati wa Lazio na Itali Jorginho, 26. (Manchester Evening News)

City pia imembishia hodi kiungo wa kati wa Real Madrid na Croatia Mateo Kovacic, 24, huku wakiwa na wasiwasi kuhusu kumtia mkobani Jorginho. (Mirror)

Wilshere ajiunga na West Ham, Torreira na Guendouzi 'waelekea' Arsenal
Mshambuliaji wa Bayern Munich na Poland Robert Lewandowski, 29, anatarajiwa kusalia na klabu hiyo licha ya kuhusishwa na uhamisho (Bild)

Mkurugenzi wa michezo katika klabu ya Roma Monchi anasema kuwa ataangazia maombi ya kumuuza kipa wa Brazil Alisson lakini kufikia sasa hakuna klabu iliowasilisha ombi la kumnunua mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 25. (FourFourTwo)

Manchester United na Real Madrid wamekutana na maafisa kutoka Lazio kujadili uhamisho wa kiungo wa kati wa Serbia mwenye umri wa miaka 23 Sergej Milinkovic-Savic. (Il Messaggero - via Talksport)

Southampton ina matumaini ya kukamilisha mkataba wa £18m kumnunua beki wa Borussia Monchengladbach na Denmark Jannik Vestergaard, 25. (Daily Echo)

Newcastle United ina matumaini ya kumsajili kwa mkopo winga wa Chelsea Kenedy kabla ya klabu hiyo kuelekea Ireland baadaye wiki hii. Mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 22 raia wa Brazil anaelekea Tyneside kukamilisho uhamisho wa mkopo (Newcastle Chronicle)

Borussia Dortmund inapanga kutumia fedha walizopata baada ya kumuuza mshambuliaji wa Ukraine Andriy Yarmolenko aliyeelekea West Ham ili kusaidia kufadhili uhamisho wa Wilfried Zaha, 25, kutoka Crystal Palace ambaye amevutia hamu kutoka klabu za Tottenham na Everton baada ya kukataa mkataba mpya katika klabu ya Selhurst Park. (Sun)

Kutoka BBC

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic