July 10, 2018

Jerryson Tegete akisaini mkataba wa mwaka mmoja na Kagera
Na George Mganga


Aliyekuwa mshambuliaji wa Majimaji FC msimu uliopita, Jerryson Tegete, amejiunga na Kagera Sugar kwa kusaini mkataba wa mwaka mmoja. 

Tegete amefikia mwafaka na viongozi wa Kagera kuweka saini hiyo na sasa atakuwa sehemu ya kikosi cha Kagera msimu ujao.

Ukiachana na Tegete, aliyekuwa kipa namba moja wa Ndanda FC, Jeremiah Kisubi naye amemwaga wino kwa kusaini mkataba wa mwaka mmoja wakata miwa hao wa Kaitaba, Kagera.

Kipa Jeremiah Kisubi akisani Kagera mwaka mmoja kutoka Ndanda

Kagera ambao wameonesha nia ya kuibomoa Ndanda kwelikweli baada ya kumalizana na kipa wake, vilevile wameweza kumsainisha mwaka mmoja aliyekuwa Nahodha wake msaidizi, Khemed Khoja.

Khoja anacheza nafasi ya beki akiwa na uwezo wa kumudu namba 4, 5 pia namba 6 akipanda kama kiungo mkabaji.

Hemed Khoja kutoka Ndanda akisaini mkataba wa mwaka mmoja na Kagera
Achana na Khoja, wakata miwa hao wameingia mkataba wa mwaka mmoja na kiungo mshambuliaji, Majid Khamis aliyekuwa akikipiga Ndanda Ndanda FC iliyopo Mtwara.

Majd Khamis kutoka Ndanda 
Aidha, Mshambuliaji Omary Mponda naye kutoka Ndanda amekamilisha uhamisho wake kwa kusaini mwaka mmoja na Kagera.

David Luhende aliyekuwa akikipiga na Mwadui FC, naye amemwaga wino wa mwaka mmoja na Kagera.

Pia beki wa kati Amad Waziri kutoka Ndanda FC naye amesaini mkataba wa mwaka mmoja kukipiga ndani ya Kaitaba na Kagera Sugar.


0 COMMENTS:

Post a Comment

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV