July 21, 2018






Mshambuliaji wa zamani wa Simba, Laudit Mavugo hatasajiliwa tena na Baroka FC ya Afrika Kusini, kama ilivyokuwa imepangwa.

Baroka FC anayochezea Mtanzania katika ngazi ya Ligi Kuu Afrika Kusini, ilionyesha nia ya kumpata Mavugo, raia wa Burundi.

Mmoja wa maofisa wa Baroka FC, ameiambia SALEHJEMBE, wameshangazwa na Mavugo.

"Unajua kila tukimuita anasema anakuja. Tukimuita tena anasema anakuja lakini hatokei.

"Kuna wakati aliahidi hadi siku lakini hakutokea. Tumeachana naye na tumesajili mchezaji mwingine, naye anatokea Burundi."



1 COMMENTS:

  1. Mavugo hana bahati. Alipotakiwa sana na Simba miaka ya nyuma alidengua miaka 2 hakutokea. Alipotokea hakuweza kuridhisha kiu ya waliomtaka wakaachana. Sasa inaelekea shida bado ileile.

    ReplyDelete

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic