July 21, 2018





Baada ya kukamilisha zoezi la kumbakiza beki Kelvin Yondani, mwenyekiti wa zamani wa klabu hiyo, Abbas Tarimba amewashukuru baadhi ya watu akisema walifanikisha zoezi hilo.

Tarimba amesema aliowarushia shukurani hizo ni wale waliokuwa sehemu ya kufanikisha suala hilo.

“Pamoja na hivyo, kiukweli niwashukuru baadhi ya watu waliofanikisha usajili wa Yondani Yanga ambaye kwenye msimu ujao tutakuwa naye ambao ni kundi la WhaatsAp la Yanga Viva na mtu mmoja ambaye ni shabiki mwenye mapenzi na timu yake, jina lake maarufu ni Yanga Makaza anayeishi mkoani Mwanza.

“Pia nimshukuru Yondani mwenyewe ambaye ni muhimili mkubwa katika timu kwa kufanikisha usajili wake pamoja na kaka yake, Sunday ambaye ni meneja wake.

"Bila kuisahau familia ya Yondani ambayo imefanikisha kubakia, hivi sasa ninaelekeza nguvu kwa Kessy ambaye naye nilifanya naye mazungumzo ambayo yamefikia pazuri wakati wowote tutalimaliza hilo,” alisema Tarimba.


0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic