July 11, 2018

KIUNGO Mohammed Issa Banka, jana alikamilisha usajili wake wa kujiunga na Yanga kwa mkataba wa miaka miwili akitokea Mti­bwa Sugar.


Banka ambaye alikuwa ak­iwindwa na Yanga na Simba, amefanikisha usajili huo jana Ju­manne na kutambulishwa mbele ya waandishi wa habari katika Makao Makuu ya Klabu ya Yanga jijini Dar.

 

Akizungumza baada ya kuka­milisha usajili huo, Banka alisema: “Namshukuru Mungu kwa jambo hili na nawashukuru Yanga kwa kunipokea vizuri.

 

“Nimekuja hapa malengo yangu ni kufanya vizuri na kuifikisha Yanga mbali zaidi. Nimejipanga vizuri kushindania namba na naamini nikifanya mazoezi kwa juhudi kubwa nitafanikiwa tu.”


Naye Mwenyekiti wa Kamati ya Usajili ya Yanga, Hussein Nyika, alisema: “Usajili huu wa Banka ni mzuri kwetu na hakuna ambaye hamfahamu mchezaji huyu. Eleweni tu tumemsajili kwa miaka miwili, suala la kiasi gani tumem­patia hilo linabaki kuwa siri yetu kwani maslahi ya mtu hayawekwi wazi.”Wakati Banka akitambulishwa, Championi pia lilimshuhudia kiungo, Deus Kaseke akiingia klabuni hapo jana kwa ajili ya ku­kamilisha usajili wake wa kujiunga na Yanga akitokea Singida United.Pia Mrisho Ngassa na Heritier Makambo raia wa DR Congo, nao walifika klabuni hapo jana kwa lengo la kusaini mikataba baada ya kocha mkuu wa kikosi hicho, Mcongo, Mwinyi Zahera, kuwaku­bali.

0 COMMENTS:

Post a Comment

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV