July 11, 2018


Uongozi wa klabu ya Yanga umefunguka kuhusiana na usajili wa kiungo mshambuliaji, Issa Mohammed Banka aliyetia kandarasi ya miaka miwili na mabingwa hao wa kihistoria katika Ligi Kuu Bara.

 Kupitia Mwenyekiti wa Kamati ya Usajili Yanga, Hussein Nyika, amesema kuwa mchezaji huyo waliyemsajili kutokea Mtibwa Sugar amekuwa na mchango mkubwa ndani ya Uwanja. 


 Nyika ameeeleza kuwa hakuna asiyejua mchango wa Banka kutokana na umahili wake wa kutandaza soka kuwalisha mipira washambuliaji wa mwisho, kitu ambacho kimepelekea wao kumsajili. Aidha, Nyika anaimani Banka atakuwa msaada ndani ya kikosi cha Yanga ambacho kinajiandaa hivi sasa kuelekea mchezo wa Kombe la Shirikisho dhidi ya Gor Mahia FC ya Kenya. 

 Kuelekea mechi hiyo kubwa ya mkondo wa kwanza, Yanga itasafiri kwenda kuanzia Kenya ambapo itacheza dhidi ya mabingwa hao watetezi jijini Nairobi Julai 18 2018.

3 COMMENTS:

  1. Hivi mbona ni mchezaji mmoja tu amekuwa publicized kama vile mmesajili wachezaji wa 5???

    ReplyDelete
  2. Hivi mbona ni mchezaji mmoja tu amekuwa publicized kama vile mmesajili wachezaji wa 5???

    ReplyDelete

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV