July 11, 2018



Wakati hao wakishangazwa na Tarimba kujiondoa, wengine pia wamefunguka na kusema uongozi wa Yanga umekuwa hauna watu wa mpira kitu ambacho kimesababisha Tarimba kujiondoa.

Tarimba mabaye aliteuliwa kupitia Mkutano Mkuu wa Yanga Juni 10 2018, juzi alitangaza kujiuzulu nafasi hiyo kutokana na kutokuwa na maelewano na baadhi ya viongozi wa Yanga katika kutekeleza majukumu ya Kamati aliyopewa.

Tarimba alieleza kuwa viongozi wa Yanga ni waongo hivyo ni vema wakamuacha aendelee na mambo yake mengine kutokana na namna mwenendo wa sehemu hizo mbili baina yake na Yanga unavyoenda kutokuwa sawa.

1 COMMENTS:

  1. Hivi mnaposema uongozi wa Yanga hauna watu wa mpira ninini hasa mnachomaanisha? Katibu Mkuu wa Yanga alikuwa mchezaji mpira kuanzia klabu ya Mseto Morogoro, Mkoa wa Morogoro, Forest Hill sekondari, Yanga , Taifa Stars, Kocha timu ya Taifa. Huyu ndiye Mtendaji Mkuu wa Klabu ya Yanga. Hivi mpira upi mnaotaka uongozi uwe nao? Abbas Tarimba kacheza wapi mpira? mbona haambiwi sio mtu wa mpira? Inaelekea neno hili linalengwa kutumika kwa watu fulanifulani msiowapenda lakini tunakosea. Kama ni kiongozi tuliyemchagua wenyewe iweje leo tuwaone sio watu wa mpira? Tuvumilie muda ufike tufuate taratibu tuchague wengine tutakaoona wanafaa. Tusiwaseme vibaya waliopo sasa tunakosea.

    ReplyDelete

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic