July 17, 2018


Na George Mganga

Mshambuliaji wa kimataifa wa klabu ya Simba, Mganda, Emmanuel Okwi, amerejea nchini na tayari ameshajiunga na wachezaji wenzake kujinoa kwa ajili ya msimu ujao wa Ligi Kuu Bara.

Okwi alisafiri kwenda Uganda kwa ajili ya mapumziko baada ya msimu wa Ligi Kuu 2017/18 kumalizika kutokana na uongozi klabu kutoka likizo kwa wachezaji wote wa kikosi cha kwanza.

Ujio wa Okwi unakuwa unakutanisha na straika mpya hatari aliyesajiliwa hivi karibuni kutoka Gor Mahia FC ya Kenya, Meddie Kagere, ambaye alianza kutema cheche zake katika mashindano ya KAGAME.

Mbali na Kagere, Okwi atakuwa anacheza sambamba na Adam Salamba pamoja na Marcel Kaheza ambao pia wamesajiliwa baada ya msimu wa ligi kumalizika na kushiriki michuano ya SportPesa Super Cup nchini Kenya.

Kikosi cha Simba kimekuwa na ratiba ya mazoezi ya kujiandaa na msimu mpya jijini Dar es Salaam yanayoendelea kwenye Uwanja wa Boko Vetrani.




1 COMMENTS:

  1. Nadhani Simba wanaenda vizuri mpaka hivi sasa kwani katika miaka ya hivi karibuni tumekuwa tukishuhudia Simba ikibadili wachezaji kadhaa karibu kila msimu. Lakini timu yao ilioshiriki mashindano ya Afrika na ile iliowapa ushindi wa ligi kuu bara karibu wote wapo ni jambo zuri kuwa na kikosi kilichokaa pamoja kwa muda mrefu. Ni matumaini yetu Simba kufanya vizuri zaidi mwaka huu hasa kunako mashindano ya kimataifa. Kwa upande mwengine bila kumumunya Simba imebeba vijana wengi chipukizi wenye vipaji vya hali ya juu ingekuwa vizuri hawa vijana wakaondoa uoga na kuwa na uthubutu wa kuonesha uwezo kamili bila aibu wachukue mifano ya wachezaji vijana kwenye mashindano ya kombe la Dunia yaliyomalizika.
    ..

    ReplyDelete

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic