MANCHESTER NGUMU VS BALE, CHELSEA VS JUVENTUS: TETESI KUBWA ZA SOKA ULAYA LEO
Manchester United huenda wakakosa kumsaini Gareth Bale wakati mshambuliaji huyo kutoka Wales mwenye miaka 29 anatarajiwa kuambiwa kuwa yuko kwenye mipango ya meneja mpya wa Real Madrid Julen Lopetegui. (Metro)
Manchester City hawataki kutimiza ofa ya Real Madrid ya pauni milioni 80 kwa kiungo wa kati raia wa Croatia mwenye umri wa miaka 24 Mateo Kovacic. (Sky Sports)
Chelsea wanazungumzia mipango ya kumnunua mshambuliaji wa Juventus raia wa Argetina Gonzalo Higuain, 30 kwa pauni milioni 53. (Evening Standard)
Newcastle na Celtic wanammezea mate kiungo wa kati wa Uruguay Giorgian de Arrascaeta, 24, ambaye thamani yake imewekwa kuwa milioni 18 na Cruzeiro. (Sun)
Monaco wametangaza ofa kwa CSKA Moscow kwa kiungo wa kati mrusi mwenye miaka 22 Aleksandr Golovin, ambaye pia amehusishwa na ofa ya pauni milioni 22 ya kuhamia Chelesea. (Sport Express - in Russian)
Southampton wamejitenga kutokana na ripoti kuwa wanamwinda mchezaji wa Liverpool mwenye miaka 25 raia wa England Danny Ings. (Daily Echo)
Meneja wa Arsenal Unai Emery anapanga kukipunguza kikosi chake na hatma ya mshambuliaji wa Engaland Danny Welbeck, 27, na kipa raia wa Colombia David Ospina, 29, hazijulikani. (Telegraph)
Kutoka BBC
0 COMMENTS:
Post a Comment