July 20, 2018


Straika hatari wa zamani aliyewahi kuichezea Yanga, Mkenya, Boniface Ambani, amesema kiwango cha timu hiyo namna ilivyocheza dhidi ya Gor Mahia FC haukuwa unaendana na ukubwa wa klabu.

Katika mchezo huo wa Kombe la Shirikisho Afrika uliopigwa Jumatano ya wiki hii jijini Nairobi, Kenya, Yanga waliruhusu nyavu zao kutikishwa mara nne bila majibu na Gor Mahia ambao ni mabingwa watetezi wa ligi nchini humo.



Kwa mujibu wa Radio EFM, Ambani ameeleza kuwa Yanga haikuonesha kiwango kinachoendana na ukubwa wa klabu na inapaswa kufanya usajili wa maana ili kuepusha aibu.

Ambani ambaye aliwahi kutamba na Yanga miaka ya 2000 akiwa kwenye kikosi hicho mwaka 2009 amesema kikosi kinapaswa kufanyiwa maboresho tofauti na wachezaji aliowaona kutokuwa na uwezo wa kutosha.

Mbali na uwezo, Ambani amefunguka kuwa aliongea na baadhi ya viongozi wa Yanga na wakamdokezea kuwa wachezaji hawajalipwa mshahara, jambo ambalo linaweza likawa limepelekea kuambulia kichapo hicho cha mchezo wa mkondo wa kwanza.

Ambani amesema aliambiwa wachezaji kadhaa bado hawajpokea stahiki zao huku wengine wakibaki Dar es Salaam wakigomea kusafiri wakiomba kuongezewa mikataba mingine ili waendelee kuichezea timu.

Hassan Kessy na Kelvin Yondani ni wachezaji waliobaki nchini wakati kikosi cha Yanga kikisafiri kuelekea Kenya kwa ajili ya mchezo dhidi ya Gor Mahia.

3 COMMENTS:

  1. Aisee kwa staili hii basi Yanga ni mwendo wa chura na kwa kweli tutapata tabu sanaa.Wapi kina mzee Akilimali waokoe jahazi?

    ReplyDelete
    Replies
    1. Huyu mzee Akilimali ndio alikuwa mstari wa mbele kumtolea mbovu Manji na eti anataka uenyekiti wa klabu na sasa anatakiwa aonyeshe uwezo wake wa kuendesha klabu.Kuanguka kwa Yanga ni kuporomosha kiwango cha soka kwa Taifa hili kwa maana tunahitaji klabu madhubuti ili kuleta ushindani na Simb, Azam, na timu zingine kwenye VPL vinginevyo ufalme wa soka Tanzania utabakia kwa Simba na Azam.Chonde-chonde wanayanga

      Delete
  2. Kama Manji hayupo ina maana yanga hawana plan B . hebu tuachen uzwazwa. Kama ingetokea manji karud kwao india au canada au vinginevyo ndo kifo cha yanga au?

    ReplyDelete

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic