July 20, 2018

Beki wa kati wa Yanga, Kelvin Yondani

NIMESIKIA beki wa kati wa Yanga, Kelvin Yondani amekuwa katika mazungumzo na klabu yake tayari kwa ajili kuongeza mkataba mwingine.
Achana na zile taarifa zilizoandikwa na magazeti (si Championi) kwamba ameishajiunga na Simba kwa miaka miwili. Simba tayari walilieleza Championi kuwa kwa msimu ujao, hawakuwahi kuwa na pendekezo la Yondani.

Walieleza wazi kwamba kama wangemtaka Yondani, basi wangemsajili mapema sana kwa kuwa Yanga ilishinda kumpa mkataba mpya kwa muda mwafaka kwa kuwa alimaliza mkataba muda mrefu sana.

Wakati fulani, niliwahi kuandika nikimsihi Yondani kuitumikia Yanga hadi hapo watakapokubaliana. Niliamini alitakiwa kufanya vile na kuisaidia Yanga hadi hapo watakapofikia mwafaka.

Hata hivyo, tunarudi upande wa Yondani kwamba naye kama mwanadamu anachoka. Lazima tujue ana familia na ana wazazi wake pia wanamtegemea.
Unajua, Yondani amekuwa mvumilivu na unaweza kusema amejitahidi. Sote tunakubali anapoitumikia Yanga anajituma kwa kiwango cha juu kabisa na watu wote wamekuwa wakimpongeza kwa kazi nzuri.

Sasa kitendo kinachofanyika sasa kumvurumishia matusi mtandaoni baada ya zile taarifa za uzushi kwamba amesaini Simba, nafikiri si sahihi hata kama zingekuwa na ukweli.

Kuichezea Yanga si lazima, uamuzi wa mchezaji mwenyewe kwa kuwa mpira kwake ni kazi. Bahati mbaya sana, Yondani hajachukua uamuzi kabla ya kuonyesha uvumilivu, kilichotokea ni viongozi kuahidi kwamba wangemtimizia ahadi kwa kumpa fedha wakati fulani, lakini haikuwa hivyo.

Hapa si kwamba nawalaumu viongozi, natambua nao wako katika hali ngumu na wanaendelea kupambana kuhakikisha mambo yanakwenda sawa ingawa nimekuwa nikihimiza suala la umoja na ubunifu kitaalamu kufanikisha mambo.

Wale wanaomtukana Yondani ninaamini wengine wanakuwa ni watu wa makundi haya mawili. Inawezekana hawana familia na wanaishi nyumbani kwao au ni watu ambao wana familia lakini bado hawajaelewa maana ya kazi hasa ni jambo lipi.

Katika kundi hili la kwanza, hawa watu hushindwa kuelewa kwamba anayekuwa ofisini hutaka kupata maslahi ofisini kwake kama ambavyo mjomba wake (kama anakaa kwa mjomba), anavyopambana kupata fedha za kuendesha familia akiwemo yeye.

Yondani ana familia, lazima awe na kipato k i t a k a c h omu w e z e s h a kuiendesha familia yake. Hivyo suala la kuhakikisha analipwa vizuri wala si mjadala tena.

Kundi la pili ni lile ambalo huona mwanasoka ni mtu anayejifurahisha au mtu anayetoa msaada tu. Wako wanaona mwanasoka ni mtu anayepaswa kucheza tu lakini hakuna shabiki anayepigania maslahi yake anaposikia hajalipwa.
Iko haja ya kujifunza kwamba wanasoka nao ni wanadamu wanahitaji maslahi yao ili kuendeleza maisha yao. Hakuna upendo wa kutoka upande mmoja uliopdumu milele.

Mara kadhaa nimeandika makala kuwasihi wachezaji wa Yanga kuwa na subira ili kuisaidia timu yao. Lakini najua na ndiyo maana leo nimeandika kwamba nao ni binadamu na wana mahitaji yao. Hivyo kama kuna sehemu wamefanya uvumilivu, wakati mwingine pia wanachoka.

Hivyo si sahihi kumtukana Yondani kwa kuwa kuna taarifa kaenda Simba, ambazo si kweli. Si sahihi kumvurumishia maneno makali na machafu eti kwa kuwa amegomea kuichezea Yanga.

Inawezekana ikawa vizuri kufikisha ujumbe kwa viongozi wa Yanga kuwaambia wampe Yondani anachohitaji na kama ni kikubwa, wafanye juhudi za kumpata na kuzungumza naye ili kumalizana naye kama walivyoanza kufanya.
Yondani kaifanyia Yanga mambo mengi sana, huenda maumivu ya upendo wake kwa Yanga ni makubwa sana hata kuliko yule anayetukana akitaka watu wamuone.

Si kila mwenye nafasi ya kuwa na akaunti ya mtandao wa kijamii anaweza kutukana na kusema watu hovyo. Mjifunze, badilikeni na acheni umbumbu wa mitandao ya kijamii.

9 COMMENTS:

  1. Acha kutuandikia pumba zako. Umekuwa unaandika habari za uongo sana na kujia kujidai kukanusha. Habari za Yondani ulizaandika sana wewe leo hii unatengeneza tena nini ili uonekane tu punguza upuuzi utajenga jina. Umeshindwa hata kutupa matokeo ya Cecafa ya wadada wetu unaandika upuuzi wa Yanga na Simba tu. Bila Yanga na Simba wewe huna cha kusema siyo au ndizo timu pekee Tanzania? Badili mfumo wa habari zako.

    ReplyDelete
    Replies
    1. HAWA SI NDO WANAMILIKI YALE MAGAZETI YA IJUMAA WIKIENDA NA UWAZI..KWAHIYO UMBEA NA UZUSHI WAO WALISHAZOEA SANA..mimi nilishasema nikikutana na muandishi wa hii blog na nyoka naanza kuua muandishi na Nyoka namuacha aende kwa sababu wamekua wanaandika taarifa halafu wanafanya kazi za kukanusha ,wiki iliyopita habari walioiandika sana ilikuwa ni YONDANI ASAINI SIMBA MIAKA MIWILI, MARA YONDANI AMEENDA SIMBA KIMAFIA..leo hii walivyokuwa WASENGE wamesahau eti wanasema sio wao, walioandika habari hiyo wamesahau na lile gazeti la SPORT XTRA ni lao. Mimi sijapata kuona waandishi MAFALA kama hawa wa blog hii.

      Delete
  2. yote kwa yote wapenda soka tunakitu cha kukumbuka kutoka kwa KELVIN YONDAN unafiki tuweke pembeni

    ReplyDelete
  3. Mtemea makohozi wachezaji wenzie anahitaji heshima

    ReplyDelete
  4. Yanga hakuna haja ya kumlipukia mwandishi au hii blog kwani alichoandika muandishi ni sahihi kabisa kuhusu Yondani. Blog hii ni miongoni mwa blog inayojitahidi sana kutuhabarisha kwa wakati sidhani kama kuna blog nyengine Tanzania inayofutalia mechi nyingi za soka zinaazochezwa na kuzirusha laivu. Mashabiki na wadau wa Yanga mnapaswa kukumbuka blog hii ilipigia kelele sana kitendo cha baaadhi ya viongozi wa Yanga kumbeza Yusufu Manji na kupinga suala la uekezaji kwenye timu na hali inayoendelea ya ukata pale yanga ndio sababu ya muandish au waandishi kunyanyua sauti zao kutaka isitokee yanayotokea sasa pale yanga yaani ni aibu tupu. Yanga haina mipango yeyote ile ya kujiendesha tofauti na Simba ambapo hata kabla ya kuja Mo tayari ilikuwa na vyanzo kadhaa vya mapato. Tangu hapo awali Simaba kuliundwa kundi la Friends of Simba ili kuepusha suala timu kumtegemea mtu mmoja. Simba wanasiku yao ya Simba day ambayo Jezi mpya za msimu huzinduliwa na sambamba kutambulishwa kwa wachezaji wapya kunako chochea uzwaaji wa jezi pamoja na mapato ya mlangoni siku ya mechi. Kuna mambo mengi sana kutoka SIMBA timu nyingi sana hapa nchini si yanga hata nyengine kuiga. Pale Yanga Kuna watu wajinga na kuwaambukiza ujinga huo wafuasi wao. Kwanini kusikuwepo na friends of Yanga? Kwanini hakuna yanga day? Kwanini hakuna ubayana au uwazi wa miradi ya Yanga inayoweza kuchangia mapato? Kwanini kusikuwepo na mkataba wa ushirikiano na benki fulani kuwashirikisha wataalamu wa masuala ya uchumi na hakiba jinsi ya kujiwekea hakiba? Kwanini wakatae uwekezaji klabuni? Watu wa yanga wana mengi ya kuhoji viongozi wao badala ya kuwatukana na kuwakarapia waandishi wanaojaribu kufichua uozo kwenye timu yao.

    ReplyDelete
  5. Mchezaji yeyote yule na niseme binadamu wote wanastahili heshima. Isipokuwa yeye mwenyewe lazima atunze heshima yake. Akifanya mambo ya kihuni hawezi kuheshimiwa. Sasa kwa Yondani kama unadhani hakuheshimiwa basi jiulize mambo gani ya ovyo amefanya hadi watu walewale waliokuwa wakimuheshimu sasa wameacha kumuheshimu?? Ni matendo yako ndiyo yanabeba karata ya kuheshimiwa au kutoheshimiwa.

    ReplyDelete
    Replies
    1. Mifano miwili kwa Yondani. Kumtemea mate mchezaji mwenzie ni kitendo cha OVYO sana. Kimemuondolea heshima. Kuisusa Yanga kwenye mechi muhimu za kimataifa pamoja na hii ya Gormahia huku akiwa Nahodha Msaidizi lakini ndie Nahodha uwanjani kumempunguzia heshima. Hivi angeenda kucheza huku akiwa andai mkataba mpya huoni kama angekuwa mzalendo kwa timu yake?

      Delete
  6. Kumbe anaedai haki yake hujipunguzia heshima. Jee wewe ungelikuwa mfanya kazi bila ya kulipwa. Hilo ungekubali? Kaka hilo ni porojo

    ReplyDelete

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic