July 14, 2018




Nestor Pitana ndiye Mwamuzi atakayechezesha mechi ya fainali ya Kombe la Dunia kati ya Croatia dhidi ya Ufaransa kesho Jumapili nchini Urusi.

Pitana aliwahi kuwa mwigizaji maarufu nchini Argentina na sasa ni mwalimu wa mchezo wa sarakasi.

Katika Kombe la Dunia Urusi aliichezesha Croatia ikiivaa na kuishinda Denmark.

Alianza kuwa mwamuzi mwaka 2007 na baada ya miaka mitatu akabeba beji ya FIFA.

SIFA ZAKE

1. Ni moja ya waamuzi walio hatari zaidi katika kufanya maamuzi Uwanjani, huwa hapepesi macho katika hukumu ya penati endapo itakuwa imestahili.

2. Ana sifa kubwa ya kutoa kadi za njano na nyekundu kwa wingi zaidi bila kujali ni wangapi wamezipata katika mechi husika.

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic