July 14, 2018


Kipute cha michuano ya Kombe la Dunia kinaendelea tena leo kwa mshindi wa tatu kusakwa nchini Urusi baina ya England na Ubelgiji.

Ubelgiji wanakutana na England kwa mara ya pili kwenye michuano hii mwaka huu baada ya kucheza katika hatua ya makundi na England kupoteza kwa bao 1-0.

Kabla ya England kupoteza mechi ya mwaka huu hatua ya makundi, ilipoteza pia mechi moja kati ya 21 ilizokutana na Ubelgiji huku zikienda sare mara 5.

Ubelgiji na England zimeweka rekodi ya kukutana mara mbili kwa mara ya kwanza kwenye Kombe la Dunia nchini mwaka huu ambapo iliwahi pia kutokea kwenye fainali za 2002 Brazil kucheza mara mbili dhidi ya Uturuki.

Ubelgiji inaingia kucheza na England baada ya kupoteza mchezo wa nusu fainali kwa bao 1-0 dhidi ya Ufaransa na England iking'oka kwa kupoteza kwa mabao 2-1 dhidi ya Croatia.




0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic