July 23, 2018


Zikiwa zimesalia siku 3 pekee kwa dirisha la usajili kwa wachezaji Tanzania kufungwa, imeelezwa kuwa Rais wa klabu ya Singida United amekubali kuwaachia Yanga mchezaji Feisal Abdallah 'Fei Toto' kwa sharti moja.

Usajili wa Toto ulizua gumzo baada ya kutambulishwa na timu mbili ndani ya siku moja na kuleta sintofahamu kuhusiana na namna alivyomalizana na viongozi wa pande mbili za klabu hizo.

Kutokana na mkanganyiko huo, Nchemba amekubali yaishe lakini akiwataka Yanga kulipa gharama za usajili wa Toto kiasi cha shilingi milioni 18.

Nchemba amewataka Yanga kulipa fedha hizo ambazo tayari zimeshatolewa kwa Toto baada ya kumalizana na Singida na kukubaliana kusaini mkataba wa miaka mitatu.

Singida United ndiyo walikuwa wa kwanza kumtambulisha Toto majira ya asubuhi ya Julai 12 2018 na baadaye majira ya saa 11 Yanga nao wakambulisha wakisema amesaini miaka miwili.


3 COMMENTS:

  1. ndio madhara ya timu za mikoani kuchukua viongozi wenye mapenzi na timu kubwa ndio maana yanga walimchukua mchezaji huyo wakijua kabisa kuwa wana mtu wao singida ambaye atawapa huyo mchezaji matokeo yake singida itakosa sapoti ya watu wenye mapenzi na simba kwani wationa timu hiyo ni tawi la yanga historia ya toto itajirudia

    ReplyDelete
    Replies
    1. Mwigulu amepimwa Na kugundua walikurupuka kumsainisha mchezaji mwenye mkataba, wao singida wakikomaa Na Fei Na JKU nao wakikomaa kwenda kwenye mamlaka husika kwa kesi ya mchezaji wao kurubuniwa Na kusaini Timu nyengine huku akiwa Ana mkataba wenye zaidi ya miezi sita, itakua ishu Na Singida wataadhibiwa so inabidi wawe wapole tu.

      Delete
  2. Kwani inauma nyi tawi lenu SI lipuli?? au mkuki kwa nguruwe acheni umbulula wenu

    ReplyDelete

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic