July 8, 2018


Mabingwa wa kihistoria katika soka la Bongo, Yanga, imeanza kujibu kujibu mapigo ya watani zao wa jadi Simba kwa kunasa saini mpya za wachezaji wawili.

Wachezaji hao ni beki wa kulia Juma Abdul ambaye ameongeza mkataba wa mwaka mmoja kuendelea kuichezea klabu hiyo na kuzima ndoto za kuelekea Azam kama ambavyo awali ilikuwa ikitajwa.

Abdul aliingia katika tetesi za kuhusishwa kutua Azam lakini mabosi wa Yanga kupitia Kamati ya Usajili imejitahidi kuwapiga kete matajiri hao na kumalizana naye kwa kumuongezea mwaka mmoja.

Mbali na Abdul, Yanga imefanikiwa kumrejesha kiungo wake mjanja Deus Kaseka ambaye waliwahi kumsajili akitokea Mbeya City na baadaye kutimkia Singida United ya Singida.

Kaseke amerejea Yanga na kusaini kandarasi ya mwaka mmoja pia sawa na Abdul ambaye ameongeza muda huo katika harakati za kujiandaa kuelekea msimu ujao wa ligi.

Taarifa za ndani kutoka Yanga ukiachana na Abdul pamoja na Kaseke, inaelezwa Kamati ya Usajili ipo kwenye mazungumzo na beki Andrew Vincent pamoja na kipa Beno kakolanya kwa ajili ya kusaini kandarasi mpya na muda wowote wanaweza wakamwaga wino.

11 COMMENTS:

  1. Unarejea kutoka kuwa nahodha na kuewa kandarasi ya mwaka mmoja? unless kuwe na vipengele zaidi juu ya mkataba huo kama ni kweli

    ReplyDelete
  2. Hapa inatia wasiwasi na lipo suala la kujiuliza nalo, ni kwanini ikawa mkataba wa mwaka tu? Inaonesha hao jamaa ni kama walilazimishwa na kukubali mwaka mmoja tu kwa shingo upande pia huenda yanga ikawa imeridhia kwakuwa hawana hela ya miaka miwili isipokuwa mmoja tu na pia kuwarifhisha wachezaji wasije wakakwama muda wa miaka miwili bila ya malipo na huku sheria haiwawezeshi kuonfoka. Simba wamempa Wawa mwaka mmoja tu kwa kuhofia uwezo kutokana na umri wake. Namuuliza muandishi kutokana na usemi wake kuwa Yanga eti wamejibu mapigo kwa simba, ni mapigo gani hayo na kwaninipaka leo hatujasikia kuhusu Kesi, Yondani na wengi wengine?

    ReplyDelete
  3. Azam hawakuwa na haja nae ya ukweli Juma Abduli msitutanie hapa Yanga ana ubavu gani wa kuizidi kete Azam kwenye kukombania mchezaji?

    ReplyDelete
  4. Mwandishi kaandika kishabiki tu sababu usajili wa mchezaji asiyetakiwa azam tena usajili Wa mwaka mmoja tu hauwezi kuthibitisha kuwa yanga yajibu mapigo

    ReplyDelete
  5. Yanga ikifanikiwa kuwasainisha hao wote waliotajwa bado itakuwa imenasa mmoja tu wengne ni wa hapohapo jangwani. Lakini pia kauli ya kujibu mapigo haijatumika kwa usahihi kwa sababu hakuna timu inayosajili kwa ajili timu nyingine.

    ReplyDelete
  6. Juma Abdulasingewezakwanamnayoyotekusajiliwana Azam mbele ya bekina2 bora kabisa wa timu ya taifa ya Uganda ilihali yeye abdul hata yanga hapati namba wala hategemei kuitwa timu ya taifa mbele ya beki namba 2 bora kuliko wote Africa mashariki(kapombe)

    ReplyDelete
  7. Mabingwa wa historia...na watabaki kwenye historia. Kujibu mapigo maana yake ni kufanya kinachowiana. Ni kwa nini mikataba ya mwaka mmoja...na jee wanalipwa kiasi gani.kama ni kujibu mapigo watumie basi sh mil 500 kusajili.

    ReplyDelete
  8. WAPENZI WA YANGA MSIDANGANYWE NA KUSAHAULISHWA BADO KUNA MADUDU YA USAJILI YANGA......AMBAYO WANAYANGA KWENYE MKUTANO WA WANACHAMA WAWAHOJI HASA KAMATI YA MASHINDANO NA YA USAJILI YAFUATAYO:
    1. USAJILI WA FISTON KAYEMBE
    2. USAJILI WA MBENINI MARCELLIN KOUKPO
    Kuna taarifa kuwa kumekuwepo na hitaji la 10% na pia klabu kupoteza fedha kwa kumtumia mchezaji tiketi ya ndege, malazi, na gharama nyingine halafu mchezaji mwisho kutoroka
    3. Kamati ya mashindano na sekretarieti ihojiwe kwanini George Lwandamina alibwaga manyanga
    4. Klabu ina wadhamini kwanini wachezaji wanadai malimbikizo ya mishahara?

    ReplyDelete
  9. WAPENZI WA YANGA MSIDANGANYWE NA KUSAHAULISHWA BADO KUNA MADUDU YA USAJILI YANGA......AMBAYO WANAYANGA KWENYE MKUTANO WA WANACHAMA WAWAHOJI HASA KAMATI YA MASHINDANO NA YA USAJILI YAFUATAYO:
    1. USAJILI WA FISTON KAYEMBE
    2. USAJILI WA MBENINI MARCELLIN KOUKPO
    Kuna taarifa kuwa kumekuwepo na hitaji la 10% na pia klabu kupoteza fedha kwa kumtumia mchezaji tiketi ya ndege, malazi, na gharama nyingine halafu mchezaji mwisho kutoroka
    3. Kamati ya mashindano na sekretarieti ihojiwe kwanini George Lwandamina alibwaga manyanga
    4. Klabu ina wadhamini kwanini wachezaji wanadai malimbikizo ya mishahara?

    ReplyDelete
  10. Wote mnaugua manaramonia jinsi mnavyoandika

    ReplyDelete
    Replies
    1. This comment has been removed by the author.

      Delete

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic