July 18, 2018


Na George Mganga

Shirikisho la Soka Tanzania (TFF) kupitia Bodi ya Ligi (TPLB) limetangaza ratiba mpya ya Ligi Kuu Bara kwa msimu wa 2018/19 itakayoanza Agosti 22 2018.

Mkurugenzi wa Bodi hiyo, Boniface Wambura, amesema ligi hiyo itahusisha jumla ya mechi 380 kutoka 240 ambazo zilikuwa zilichezwa msimu uliopita kutokana na ongezeko la timu.

Wambura ameeleza katika msimu wa 2017/18 ligi ilihusisha jumla ya timu 16 pekee lakini kuelekea msimu ujao kutakuwa na idadi ya timu 20 ambazo zimefanya kuwe na ongezeko la idadi ya mechi.

Ratiba hiyo inaonesha mechi zitakazoanza Agosti 22 ni baina ya Simba SC dhidi ya Tanzania Prisons, Ruvu Shooting vs  Ndanda FC, Singida United United dhidi ya Biashara FC, Alliance FC dhidi ya Mbao FC pamoja na Kagera Sugar watakaocheza na Mwadui FC.

Wakati huo mechi yenye msisimko mkubwa itakayowakutanisha watani wa jadi, Simba na Yanga, itachezwa Septemba 30 kwenye Uwanja wa Taifa Dar es Salaam, ambapo Simba atakuwa mwenyeji wa mchezo huo.

6 COMMENTS:

  1. Kwenye Ligi Yanga hawajitoagi ila mashindano makubwa huwa wanajiandaa kisaikolojia.

    ReplyDelete
  2. Kama ingewezekana TFF ingezitoa tu mechi za simba na yanga... Maana yanga hawachelewi kutangaza kujiondoaa... Ama kutopeleka timu uwanjani.

    ReplyDelete
  3. Yanga Wakijitoa Bingwa Atatoka Wap?C Zitakuwa Zimebak Timu Za Wanawake Tu!

    ReplyDelete

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic