July 18, 2018






Mwenyekiti wa zamani wa Yanga, Abbas Tarimba ameamua kulichukua suala la kuhakikisha Kelvin Yondani na Hassan Kessy wanacheza tena Yanga msimu ujao.

Taarifa kutoka kwa mmoja wa Wanayanga kwenye kundi maarufu la klabu hiyo amesema Tarimba atafanya kazi ya kuhakikisha anamalizana na Yondani na Kessy ambao wamebaki Dar es Salaam wakati kikosi hicho kikipaa Nairobi kuifuata Gor Mahia.

“Tarimba ameona alichukue hilo suala, unajua ana uzoefu sana na haya masuala ya usajili. Sasa atahakikisha wanabaki,” kilieleza chanzo.

Jana, inaelezwa Tarimba alikutana na Kaimu Mwenyekiti wa Yanga, Clement Sanga na kuzungumza mambo kadhaa.

Awali, ililiezwa wawili hao walikuwa na tofauti na siku chache baadaye Tarimba akaamua kujiondoa katika kamati maalum.

Lakini kukutana kwao jana, kumeamsha matumaini mengi makubwa upande wa Wanachama wa Yanga.
Aidha, kumekuwa na taarifa za kwamba Yondani amejiunga na Simba ingawa viongozi wa Simba wamekuwa wakisisitiza suala hilo si kweli.

6 COMMENTS:

  1. Unaeandika wala hujui unachoandika unazungukazungukaa tuu

    ReplyDelete
  2. Yondani na Kessy wameisaliti Yanga. Leo Tarimba unawaendekeza hao walioisusa Yanga kwenye mashindano makubwa katika Afrika. Acheni michezo ya kuigiza. Tunaharibu Yanga yetu kwa siasa zenu mpirani. Waache waondoke kwani uwanjani watacheza na Tarimba? Wataenda wapi timu ya maana muda huu labda wakacheze Majimaji au Ndanda. Wachezaji hawawezi kuwa juu ya Klabu.

    ReplyDelete
    Replies
    1. Acha povuu wewe...mtapata taabu sanaa.

      Delete
    2. Acha povu wewe, hao wachezaji wameisaliti vipi hiyo Yanga? Wao mkataba umeisha na hawajapewa mkataba mpya, nani mwenye makosa hapo? Kumbuka mpira ndio ajira yao na wanahitaji fedha kuendesha maisha yao. Tuache ushabiki ktk maisha ya watu, hao yanga kama wanaona hao wachezaji ni muhimu kwanini wasiwape mikataba na wawalipe chao kama walivyokimbilia kumgombania yule mtoto na singida utd. Kule wamesema wamemlipa dogo chake pamoja na jku sasa inakuwaje wanashindwa kuwalipa yondani na kessy? Acheni ubabaishaji wenu na msilaumu wachezaji kwa usanii wa viongozi wenu.

      Delete
  3. Hivi tarimba anadhani anweza kuzuia usajiri ambao simba itahitaji.Kama hajui lengo ni kuwa wakimalizana na Yondani, anayefuatia kusajiriwa ni Manji na baadae Akilimali ndipo itaanza Kwa wanachama mmoja mmoja na hatimae kuifuta Yanga kabisa Katika historia ya mpira Tanzania

    ReplyDelete
  4. Moja ya kitu ambacho kinatia raha kwenye ushabiki wa mpira ni kuona watani (Simba na Yanga) kila mtu hapendi mwenzie afanikiwe angalau wanapendana sana. Simba na Yanga si maadui wala mahasimu..ila ni watani. Yote yanayozungumzwa kwa kiwango kikubwa ni utani. Mwandishi ndie aliyetuambia kuwa Yondani muda wowote kuanzia sasa anatua Simba (Yondani na Simba wamefikia patamu). Kwa kiwango kikubwa mwandishi siku hizi anaandika habari za uongo ili tu blog yake iendelee kuangaliwa na wapenzi wa mpira hasa ndugu zangu wa Simba. Mwandishi anajichanganya mwenyewe...mwisho wa yote atakanusha habari anazoaandika. Anafurahisha sana. Mengi anayoandika mwandishi huyu ni negative...kwa kuwa anajua wapenzi wa uapnde wa pili wanapenda kuckia majanga ya upande wa pili na si mazuri. Kwa sasawashabiki wa simba wana morali ya kusoma blog na vyombo mbalimbali vya habari....hawapendi kuckia mazuri ya upande wa pili...ila wanapenda kuckia ya kwao ambayo ni mazuri tu. Ndio maana hata miaka mitatu iliyopita...Yanga ndio ilikuwa timu inayopata nafasi kwenye vyombo vya habar kuliko timu zingine na ni kwa sababu ilikuwa vizuri. Sasa ni zamu ya Simba na wengine ndugu zangu msitaharuki

    ReplyDelete

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic