July 18, 2018


Uongozi wa klabu ya Ruvu Shooting umetangaza kufanya usajili wa kimyakimya bila mbwembwe kwa ajili ya maandalizi mapya ya msimu ujao wa Ligi Kuu Bara.

Kwa mujibu wa Msemaji wa timu hiyo, Masau Bwire, amesema ili kutimiza mipango yao ya kuhakikisha wanakuja na mfumo mpya wa mpapaso SQUARE, wanajipanga vema kwa kusajili kimyakimya ili waje na kishindi kikubwa.

Ruvu Shootinga wameanza usajili bila ya kuweka mabo hadharani wakiiga mbinu za Yanga ambazo walianza nazo lakini baadaye wakaamua kuanza kuweka kila kitu hadharani kutokana na mashabiki pamoja na wanachama wake kuja juu wakitaka kila kitu kiwe wazi.

Mpaka sasa Ruvu Shooting haijatangaza wachezaji ambao imeshawasajili huku siku za usajili zikizidi kuyoyoma na kukionekana ukimya mwingi ndani ya klabu hiyo hiyo.

Aidha, Bwire, ametisha Simba kwa kusema kuwa ana hamu kubwa ya kukutana nao kwenye Ligi ili awaoneshe namna Ruvu ilivyojipanga kwa msimu mpya.

Msemaji mwenye tambo nyingi za maneno ameeleza kuwa Ruvu inajipanga vilivyo kuhakikisha inakuja kuleta upinzani mkubwa kwa Simba pamoja na timu zingine kwenye ligi.

2 COMMENTS:

  1. Weweeeeh acha masihara , Simba??

    ReplyDelete
  2. Masau unataka SSC wakutandike wiki kama mwk Jana? Acha kelele zako

    ReplyDelete

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic