UAMUZI WA TFF KUONGEZA WACHEZAJI KIMATAIFA WACHUKUA SURA MPYA, MWAKYEMBE AINGILIA KATI
Ikiwa ni siku chache zimepita kupitishwa idadi ya wachezaji wa kimataifa 10 kutumika katika ngazi ya klabu za Ligi Kuu Bara kuanzia msimu ujao, Shirikisho la Soka Tanzania Bara (TFF) limesema lipo tayari kukaa na serikali,imeelezwa.
TFF kupitia Kamati yake ya Utendaji ilikaa kikao na kufikia maamuzi ya kuamua kuongeza idadi ya wachezaji wa kimataifa siku kadhaa zilizopita kutoka 7 mpaka 10.
Inaelezwa kuwa ongezeko hilo limemuibua Waziri wa Habari, Sanaa, Utamaduni na Michezo, Harrison Mwakyembe kupitia chombo fulani cha habari akisema uamuz huo ni vema ukatazamwa vizuri.
Mwakyembe amekuwa sehemu ya wale ambao wanaamini kama ongezeko hilo linaweza kuathiri wazawa na soka la Tanzania haswa kupitia timu ya taifa hivyo akaomba ni vizuri kama likaangaliwa kwa jicho la tatu.
Kutokana na kauli ya Mwakyembe, TFF imesema ipo tayari kukaa na serikali meza moja kujadili juu ya uamuzi wake ambao iliutoa wa kuongeza idadi ya wachezaji wengine watatu wa kimataifa.
TFF inatarajia kukutana na serikali zikiwa zimesalia siku 3 kuanzia leo Dirisha la Usajili kwa wachezaji Tanzania kufungwa.








Mwandishi acha uchochezi. Unapaswa kuelewa FIFA hairuhusu mambo yake kuingiliwa na serikali. Na pia ueelewe ni FIFA ndio iliyowapa ushauri TFF kuongenza wachezaji wa kigeni ili kuleta ushindani kwa wazawa na ushindani kwenye Ligi.TFF haikukurupuka na ndio maana ilipigwa kura kuamua kuongenza wachezaji wa kigeni.
ReplyDeleteMwandish mngese uyuu.
ReplyDeleteApo anajifanyaa oooh
Kwa kweli serikali inatakiwa kuwa makini na TFF kuepusha mzozo na FIFA kwani TFF inaongozwa na katiba ya FIFA na sio katiba ya Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania kitendo chochote cha serikali kuingilia maamuzi ya TFF ni suala la kutafutana muhali na FIFA. Na siku zote FIFA huwa hawana kumunyamunya wanaoamua kushusha rungu lao yaani ni wakali.
ReplyDeleteSerikali ni Mshauri wa TFF na wala si muingiliaji wa mambo ya TFF...Kenya wao wachezaji wa kigeni ni watano...na wala FIFA haijaingilia hilo. Hakuna mbinu ya kuleta ushindani kwa kuongeza wachezaji wa kigeni ila kuna mbinu ya kuongeza usimamizi wa soka letu ili liwe la kiushindani. Hakuna ushabiki kwenye hili ila TFF inafanya mambo mengi kwa kukurupuka. Wameshndwa kutafuta mbinu mbadala ya kuendeleza mpira wa Tanzania. Kikubwa ni kurudi tena na kuanza kuweka mfumo sahihi wa kuendeleza mpira wa miguu.
ReplyDeleteMpira si vita na mpira si maneno...mpira ni vitendo. Kuna baadhi ya timu hadi sasa zina wachezaji zaidi ya nane wa kimataifa..wanataka kutumia mbinu za ushawishi ili mwenyekiti sijui ndi rais wa TFF akubaliane na mbinu au ushawishi wao.
Kuna kipindi kamati ya ligi ikiongowa na mtu fulani...walipitisha kanuni ya siku moja kwa mchezaji kuchagua mechi ya adhabu baada ya kupata kadi za njano. Akaambiwa achague kwa kuwa walikuwa wanafukuzia ubingwa. Kukubali wachezaji kumi au kukataa na suala la kimantiki.Hata ukikaa na serikali sidhani kama kunaleta maana kikubwa suala limefika hapo na serikali kivizuri tu wamesema watakaa pamoja tuone
Suala la kuongezwa idadi ya wachezaji wa kigeni sio suala la simba au Yanaga au Azam. Na ni kutojitambua tu kuishauri Tanzania kuiga mfumo wa soka wa Kenya? Kama ingelikuwa riadha basi tungekubaliana Watanzania hebu tuwachungulie wakenya wanafanyaje mpaka wanatoka kakini sio katika mpira na kama kenya wana wanaruhusu wachezaji watano tu wa kigeni basi ndio maana Wao na sisi hatuchekani katika mpira. Hakuna mjadala yakwamba kweli kama wachezaji wanaosajaliwa watakuwa wa viwango na wazawa wakajitambua kutokubali kuwa wasindikazaji hapana shaka vijana wetu itawabidi wajitume ili kushindana kikamilifu. Na hapo ndipo patamu kwani mara ngapi vijana wetu wamekwenda nje kufanya majaribio wanashindwa kutokana na kuwa legelege. Mara nyingi timu inapomwita mchezaji kufanya majaribio huwa sio peke yake hukutana na wachezaji watatu au wanne wa mataifa mbali mbali kushindania namba moja sasa katika hali kama hiyo na huu mfuno wetu wa kudekeza wachezaji utatarajia kuna kijana wetu atakaekwenda kufanya majaribio nje akafuzu? Labda katika kila baada miaka 5 au 10 aneweza kutoka kijana mmoja kwa bahati na hayo sio malengo kwani tunahitaji maprofossional wengi kuja kuibeba Taifa Stars,ila hivi sasa ushindani umezidi zaidi kwenye soka Duniani. Soka ilikuwa ajira ya walalahoi lakini sio sasa watu wenye uwezo wametengeneza vitalu vya maana vya kutengeneza miche bora ya soka. Kwa kwetu sisi bila wachezaji wetu kutumia nguvu za ziada atawaona nani? Wenye kupinga suala kuongezwa idadi ya wachezaji wa kigeni waache pinge ila faida ni kubwa katika kujenga soka la ushindani kuliko hasara. Kuna wale wa Yanga wao wanapinga kwa sababu wanahofia kuzidiwa nguvu na Simba kwa kuwa wao hawana uwezo wa kusajili wachezaji wa kigeni, ni wivu na roho mbaya ya kijinga kabisa. Hata kama Simba hataruhusiwa kusajili wachezaji wa kigeni bado Yanga hawawezi kusalimika hata kidogo watakapokutana na Simba.
ReplyDeletehivi huyu mwakyembe amewahi kucheza mpira serikali haitakiwi kuingilia maswala ya mpira hasa pale yanapohusu kanuni wachezaji wetu wengi hawajitambui tazama Okwi anakuja na kuondoka lakini kiwango kilekile angalia kagere anavyopambana uwanjani halafu ujilinganishe na wakina Salamba amnao ubishoo umewajaa wakati hata michuano ya caf hajaanza kucheza angalia kina kessy wanavyodengua wakitaka mamilioni wakati kiwango chao ni cha kawaida sana awaache wageni waje kwani lazima wazawa wachezee simba na yanga na nyie si ndio mnadai simba na yanga wanaua vipaji hii itachochea ushindani na tutapata timu bora kuliko sasa hakuna ushindani wa maana tunapata timu dhaifu
ReplyDeleteKwani ni kila timu inauwezo wakusajili wacheza hao 10?mbona nyingine nyingi zitabaki nawachezaji wazawa.
ReplyDeleteMnaoshangilia maamuzi haya ya TFF kuongeza wachezaji 10 wa kigeni na kisha ikaruhusu wote wanaweza lkutumika kwenye mchezo mmoja, ndio mtakuwa wa kwanza kuizomea TFF wakati timu ya Taifa a Tanzania itakapokuwa inapokea vipigo vya mbwa koko kutoka kwa wapinzani wake. Iko hivi, Simba, Yanga, Azam FC labda na Singida United ndio timu zinazoweza kusajili mpaka wachezaji 10 wa kigeni. Ni timu hizi hizi zinazotoa idadi kubwa ya wachezaji wa timu ya Taifa. Sasa kama hawa wazawa watakosa namba kwenye timu zao ina maana timu ya Taifa itaundwa na idadi kubwa ya wachezaji kutoka timu ambazo hazishiriki michuano ya Kimataifa. Wachezaji hao watakuwa hawana uzoefu na aibu kubwa itaikumba Tanzania kwenye soka. Uamuzi huu utanufaisha vilabu lakini utaua timu ya Taifa.
ReplyDeleteHamna lolote kwa kisingizio cha kuiua Taifa Stars kutokana na kuongezwa kwa idadi ya wachezaji wakigeni kwani asilimia Samanini 80% taifa stars itanufaika tena sana kutokana na wachezaji wake kupata ushindani wa kutosha. Na kwanini? Mfano mtibwa haisajili hata mchezaji mmoja wa kigeni na itashiriki mashindano ya kimataifa sasa ni wakati wa wazawa kutoka mtibwa kuifikisha mbali mtibwa katika mashindano ya kimataifa ili kuleta changamoto kwa timu zilizosajili wageni na wakiweza basi mchezaji wa Taifa stars si lazima atokee simba au yanga. Kama mtibwa watafanya vizuri kwanini wasichukuliwe hata wachezaji 6 au saba kuunda taifa stars? Ila kwa sasa nnaamini mchezaji bora wa Stars lazima atatoka Simba au Azam na ni kutokana na wachezaji wazawa wa timu hizi kuzungukwa na maprofossional wanaowapa chngamoto za maana.
ReplyDelete