UJANJA ALIOUTUMIA KIPA WA SIMBA KUOGOPA KUTEMWA KIKOSINI
Katika hali iliyoshangaza mlinda mlango wa akiba wa klabu ya Simba, Emmanuel Mseja imeelezwa haieleweki alipo kufuatia kutopatika kupitia simu zake za mkononi.
Mseja ambaye alisajiliwa na Simba kutoka Mbao FC, inaelezwa hatokuwa sehemu ya kikosi cha Simba msimu ujao kutokana na mabosi wake kutoridhishwa na kiwango chake.
Kipa huyo ameamua kuzima simu zake zote ili mabosi wake wasiweze kumpata hewani kwa hofu ya kuogopa kutemwa wakati yeye anahitaji kuendelea kuitumikia klabu ya Simba.
Ikumbukwe Mseja hivi karibuni aliuomba uongozi wake kumpa nafasi katika mashindano ya KAGAME yanayoendelea hivi sasa jijini Dar es Salaam lakini ameikosa na badala yake kipa Ally Salim na Deogratius Munish wamepewa nafasi hiyo.
Haijajulikana mpaka sasa Mseja ameelekea wapi kutokana na kutopatikana hewani ingawa pia awali kulikuwa na taarifa zilizoripotiwa kuwa anaweza akapelekwa kwa mkopo mahala pengine.
0 COMMENTS:
Post a Comment