UONGOZI SIMBA WAELEZA SABABU ZA KUBADILI MAKOCHA KILA WAKATI, LECHANTRE ATAJWA
Na George Mganga
Uongozi wa klabu ya Simba kupitia Makamu Rais wake, Salim Abdallah 'Try Again' umefunguka juu ya kushindwa kukaa na makocha kwa muda mrefu.
Abdallah amesema klabu inapoajiri kocha yeyote muda wake unapomalizika huondoka kama ilivyokuwa kwa aliyekuwa kocha Mfaransa Pierre Lechantre.
Kauli hiyo imekuja kufuatia Simba imekuwa ikibadili makocha ambao wengi kwa takribani miaka saba ambao wengi wao wameshindwa kumaliza msimu mmoja.
Abdallah ameeleza Simba waliamua kuachana na Lechantre kwasababu aliomba nafasi ya kazi Cameroon, hivyo kwa busara kama uongozi wakaona ni vema busara ikatumika baada ya mkataba wake kumalizika.
Ikumbukwe Lechantre, alikuja nchini kuchukua mikoba ya Mcameroon, Joseph Omog aliyefukuzwa kazi kutokana na uongozi wa Simba kushindwa kuridhishwa na utendaji wake katika kikosi cha wekundu wa Msimbazi.
Baada ya kuachana na Mfaransa huyo, jana Simba imeingia mkataba na Kocha mpya, Mbelgiji, Patrick Aussems, aliyesaini mkataba wa mwaka mmoja.
0 COMMENTS:
Post a Comment