Mabingwa wa soka Tanzania Bara Simba wamemleta Kocha Mbelgiji, Patrick Aussems kuziba nafasi iliyoachwa wazi na Mfaransa Pierre Lechantre.
Kocha Aussems aliyewahi kuzinoa timu kadhaa zikiwamo za Ligi Kuu ya Ufaransa, ES Toyes AC na Stade de Reims pamoja na mabingwa wa Kombe la Shirikisho Afrika mwaka 2012, AC Leopards ya Congo yupo nchini tangu Jumapili.
Mbelgiji huyo mwenye miaka 53 na aliyecheza kama beki enzi zake za uchezaji akiwa na urefu wa futi 6 na inchi 3, aliishuhudia Simba ikiinyuka APR ya Rwanda kwa mabao 2-1 na jana pia alishuhudia tena Simba ililazimishwa sare ya bao 1-1 na Singida United. Mechi zote hizo ni za Kombe la Kagame.
0 COMMENTS:
Post a Comment