July 10, 2018


Shirikisho la Mpira wa Miguu Barani Afrika (CAF) limemfungia maisha mwamuzi wa Kenya, Aden Marwa baada ya kugundulika amepokea hongo (rushwa) nchini Urusi baada ya kunaswa kwenye kipande cha video kinachomuonesha akipokea pesa kutoka kwa mwandishi wa habari kabla hata kuanza kwa michuano ya Kombe la Dunia.

Baada ya uchunguzi huo uliyofanywa na Anas, ulimthibitisha Marwa ambaye alikuwa mwalimu wa Shule ya Sekondari ya Komotobo iliyopo Kuria East, alifanya kitendo hicho na hivyo kuondolewa. Mwamuzi huyo mwenye umri wa miaka 41 ambaye alikuwa mwalimu wa masomo ya Hisabati na Chemia alipokea rushwa ya dola za Marekani 600 sawa na (Sh 60,000) za Kenya sawa na Tsh. Milioni 1.36.

Familia ya mwamuzi huyo ambaye pia alipata bahati ya kupuliza kipyenga mashindano ya Kombe la Dunia mwaka 2014 nchini Brazil imekuwa ikikataa kupokea wageni wowote wanao watembelea kutokana na tukio hilo. Mchezo wake wa kwanza wa Kimataifa ilikuwa mwaka 2000 miachuano ya Afrika alipoisimamia Zanzibar.

Lakini pia alipata nafasi ya kusimamia michuano ya Shirikisho la Soka Afrika CAF kwa vijana waliyo na umri chini ya miaka 20 nchini Rwanda, michuano ya CHAN nchini Sudan mwezi Januari mwaka 2011 na yale mashindano ya kombe la dunia la vijana chini ya miaka 17 ili yofanyika Mexico mwezi Julai mwaka 2011.

 Hata hivyo Marwa hakuishia hapo alikuwepo kwenye mashindano ya vijana wa umri chini ya miaka 23 yanayosimamiwa na CAF yakifanyika Morocco mwaka 2012 kabla ya kushirki ile ya bara la Afrika Equatorial Guinea.


1 COMMENTS:

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic