July 20, 2018


Na Phillip Nkini

Mashabiki wengi wa soka waliitazama Yanga ilipokuwa ikivaana na Gor Mahia kwenye mchezo wa Kombe la Shirikisho Afrika juzi.

Haikuwa Yanga ile inayofahamika, haikuwa Yanga ambayo unaweza kutegemea kuwa inaweza kufanya kitu na haikuwa Yanga ambayo inaweza kukosa nafasi za wazi.

Hii ilikuwa Yanga nyingine kabisa, ilikuwa Yanga ya majaribio, ilikuwa Yanga ambayo ilimaliza dakika tisini bila kupiga shuti hata moja langoni, lakini ilikuwa Yanga ambayo haikuweza hata kukosa bao la wazi.

Yanga hii haikunyimwa penalti, haikumlalamikia mwamuzi na wala walipotoka hawakusema kuwa wamefikia kwenye hoteli ya hovyo au wamepuliziwa dawa kwenye vyumba vyao.

Hakika ilikuwa Yanga mbovu ambayo hata kama Gor Mahia wangecheza pungufu bado walikuwa wanaweza kuibuka na ushindi zaidi ya huo wa mabao 4-0 walioupata.

Hii siyo Yanga ile, hii ni timu nyingine ambayo haina muunganiko, haina safu ya ulinzi, safu ya kiungo ni mbovu na haina washambuliaji ina kocha anayesikitika kila wakati kwenye benchi.

Timu hii ya Jangwani imebakiza siku saba tu za kufufuka, usajili unafungwa Julai 27, leo ni Julai 20, kama Yanga hawatafanya kitu haya yaliyotokea juzi ndiyo yatakuwa maisha yao msimu mzima na hawatalalamika.

Yatakuwa maisha ya maumivu kwa kuwa hata wale walioko nje hawaonekani kuwa wanaweza kuisaidia sana Yanga, wanaweza kuibeba Yanga kwenye mchezo dhidi ya KMC lakini ni ngumu kuamini kuwa wanaweza kuipa Yanga pointi tatu dhidi ya Lipuli au Simba.

Yanga haina kipa imara, huu ni ukweli, Youthe Rostand hana uwezo wa kubaki kwenye timu kubwa kama Yanga anaweza kurudi African Lyon, anaweza kwenda Ndanda lakini siyo Yanga.

Rostand ni mbovu wa kuokoa krosi, ni mzito na pamoja na kwamba Yanga walikuwa wabovu ndani lakini alikuwa anaweza kufanya kitu kwenye mchezo huu mabao mawili hayakuwa magumu kwa kiwango hicho kwa kipa mzuri.

Yanga hawakuwa na safu ya ulinzi, unaweza kusema kuwa kufungwa mabao 4-0 ni kutokana na Gor Mahia kutokuwa na safu nzuri ya ushambuliaji, au kuridhika kuwa mabao hayo yanatosha lakini kwa safu ya ulinzi iliyokuwa inaongozwa na Abdallah Shaibu ‘Ninja’ haikuwa bora.

Ninja alionekana kuwa beki wa kawaida sana na alionekana kuwa hana uwezo wa kwenda na timu kama Yanga kwenye mechi kubwa kama hii, pia Juma Abdul na Haji Mwinyi walionekana hawana mazoezi ya kutosha.

Walionekana kuchoka kadiri muda ulivyokuwa unakwenda, walionekana kupunguza kasi kila wakati hapa kuna tatizo kwa kocha wa Yanga, wachezaji wake walionekana kutokuwa fiti muda mwingi kwenye mchezo huo.

Picha halisi ni kwamba kama kweli Yanga wanataka kuwa bora angalau kuleta upinzani kwenye ligi basi wahakikishe kuwa safu yao ya ulinzi ya msimu uliopita inarudi au kuhakikisha kuwa wanatafuta mabeki wanne bora wapya, kumbuka zimebaki siku saba.

Kiungo mpambanaji, Papy Tshishimbi alionekana kutafuta kila mbinu lakini alionekana hana msaada kutoka kwa wenzake, alijitahidi kuipenya lango ya Gor Mahia lakini mwisho aliishiwa nguvu, mtangazaji wa Supersport kwa wale waliotazama mechi kupitia huku alisema mchezaji pekee anayeonekana kufanya kazi yake ipasavyo ni huyu tu.

Ibrahim Ajibu, ambaye aliaminika kuwa anaweza kufanya vizuri kwenye mchezo huu mambo yake hayakuwa mazuri na kila alichofanya hakikufanikiwa huku mara nyingi akipambana kuwa mbinafsi, labda kurejea kwa Ngassa na Kaseke safu hii inaweza kuwa na moto mwingine, tusubiri kuona kama uongozi wa Yanga umejifunza kitu kwenye mchezo huu.

8 COMMENTS:

  1. Ukumbbue pia wachezaji watano wa kutegemewa wa Gor Mahia hawakuwepo kikosini kwa sababu kama za Yanga

    ReplyDelete
  2. Timu bila ya pesa, mafahamiano, wachezaji na mechi za majaribio uanaitabiria nini?. Natamani mechi yao ya kwanza Vodacom ingekuwa na Simba, Azam au Singida.

    ReplyDelete
  3. Juzi nolicheka sana pale msemaji mmoja wa yanga aliposema kuwa wao wanatumia akili wakati wa kusajili wachezaji wapya, kutokana na matakwa ya kocha na hawakurupuki kama wafanyavo simba kuchota wachezaji ovyo. Masiki Faisal kujifunga na yanga anaona kapata na wala hajui kuwa kapatwa. Lakini juzi si walitangaza kuwa wameshakubaliana na wachezaji wote, kumbe ni uwongo tu. Wallahi wanasikitisha yanga. Wangejaribu kuomba msaada kwa Mo huenda angeluwsonea huruma jwa kuwapa wachezaji angau watstu kwa mkopo. Lskini naona kwakuwa yanga Yanga wana ari na uungwana, basi wangekataa na mayusi juu

    ReplyDelete
  4. Nashangaa klabu kubwa Yanga hawatafuti plan B badala yake bado wanakuwa na ndoto za alinacha za Manji kuwa atarejea tu soon.
    Vinginevyo Yanga rudi kwenye staili ile ya Simba na wachezaji vivulana ama la sivyo wanayanga watapata tabu sana msimu huu wa ligi

    ReplyDelete
  5. Yanga bado ni timu nzuri isipokuwa walikosa mazoezi kwaajili ya mechi hizi hawakuwa fiti. Kusema kweli kujitoa Kagame ni makosa makubwa waliyoyafanya maana mashindano ya Kagame yangewapa mazoezi tosha ya kujiandaa kabla hawajakutana na Gormahia. Yamepita sasa tugange yajayo. Timu bado nzuri

    ReplyDelete
  6. Taratibu itajiimarisha mwanzo mgumu

    ReplyDelete
  7. Taratibu itajiimarisha mwanzo mgumu

    ReplyDelete

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic