July 16, 2018


Na George Mganga

Kikosi cha klabu ya Yanga kinatarajiwa kuondoka leo jijini Dar es Salaam kuelekea NNairobi, Kenya kwa ajili ya mchezo wa Kombe la Shirikisho Afrika.

Yanga itakuwa ina kibarua Jumatano ya wiki hii cha michuano hiyo dhidi ya Gor Mahia FC ukiwa ni wa mkondo wa kwanza.

Mechi ya mwisho Yanga kucheza kwenye kundi lake ilikuwa dhidi ya Rayon Sports ya Rwanda katika Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam na kwenda sare ya suluhu tasa ya mabao 0-0.

Yanga inaenda kumenyamana na Gor Mahia ikiwa na ina alama moja pekee ambayo iliipata dhidi ya Rayon kutokana na kupoteza mchezo wake wa kwanza dhidi ya MC Alger ya Algeria kwa idadi ya mabao 4-0.

Mchezo huo kwa Yanga utakuwa ni kuhakikisha inapata alama ili kuanza kujiwekea mazingira mazuri ya kusonga mbele kuelekea hatua nyingine.

Katika Kundi D, MC Alger inaongoza ikiwa na alama 4 ikifuatiwa na Gor Mahia yenye 2, na Rayon Sports ikiwa na mbili wakati Yanga ikiwa na 1 pekee.

1 COMMENTS:

  1. HIVI YANGA MBONA MNATUAIBISHA HIVI.....MIMI NITAANDIKA BARUA TFF ILI ITOE ONYO AMA KUWAADHIBISHA VIONGOZI WA TIMU ZOTE ZINAZOSHIRIKI MASHINDANO YA KIMATAIFA, KAMA HAKUNA MAANDALIZI YA KUTOSHA , NA KUWA KAMA WACHEZAJI HAWAPEWI MAANDALIZI MAZURI, MAZOEZINI, MALIPO NA MOTISHA NZURI, SAFARINI KUKOSA WACHEZAJI MUHIMU, MWISHONI KATIKA MECHI AMBAPO WANAWAKILISHA NCHI NA KUBEBA BENDERA YA NCHI.....MWISHONI KUISHIA KUFUNGWA AIBU SIO KWA YANGA TU BALI TAIFA ZIMA...RAISI MAGUFULI NAKUMBUKA ALISEMA IFIKE MWISHO TIMU ZETU ZISIWE ZINAISHIA KUFUNGWA FUNGWA TU, NI AIBU SANA...IFIKE MWISHO SASA. YANGA HAWAKUSHIRIKI CECAFA WAKISEMA WACHEZAJI WAO HAWANA MIKATABA, NA WAMEPEWA RUHUSA YA KUPUMZIKA, SASA CAF IMEFIKA NAPO BADO KUMBE HATA MIKATABA HAWAJAPEWA NA WENGINE WANAGOMA, MAJINA YA WACHEZAJI WATATU YAMECHELEWA CAF, HAYA BADO USAJILI UNASUASUA HUU NI UPUUZI MKUBWA....HAIVUMILIKI LAZIMA VIONGOZI WOTE WAJIUZULU.....TUNAKWENDA KUIAIBISHA NCHI...KUNA HAJA GANI YA YANGA KUSHIRIKI MASHINDANO HAYA IKIWA KWAMBA WANAENDA KUPELEKA KIKOSI KISICHO IMARA...WATANZANIA IMEFIKA WAKATI TUSIWE TUNATEGEMEA MIUJIZA, AU BAHATI...MPIRA NI SAYANSI NA MAANDALIZI, NA MOTISHA KWA WACHEZAJI NA BENCHI LA UFUNDI.....USANII NA USWAHILI SWAHILI UFIKE MWISHO....WAPENZI WA SOKA TANZANIA TUMECHOKA KUWA WASINDIKIZAJI NA KICHWA CHA MWENDAWAZIMU JAMANI......

    ReplyDelete

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic