July 16, 2018


Wakati kikosi cha Yanga kikitarajiwa kuondoka nchini leo, baadhi ya wachezaji hawatakosekana katika msafara wa timu hiyo.

Hassan Kessy pamoja na beki Kelvin Yondani ndiyo wachezaji pekee watakaobaki Dar es Salaam kutokana ambao wameelezwa hawakuwa kambini na Yanga.

Kwa mujibu kwa Ofisa Msaidizi wa Habari Yanga, Godlisten Chicharito , amesema Kessy na Yondani hawakuwa kwenye ratiba ya mazoezi na Kocha Mwinyi Zahera hivyo hawatoambtana na timu kuelekea Kenya.

Awali ilielezwa kuwa Yondani na Kessy wamegoma kusafiri na timu ikielezwa wanashinikiza kuongezewa mkataba wa kuendelea kuichezea Yanga lakini uongozi umeibuka na kueleza tofauti.

Aidha, wachezaji Heritier Makambo, Mrisho Ngassa na Deus Kaseke waliosajiliwa hivi siku kadhaa zilizopita hawatokokuwa sehemu ya kikosi dhidi ya Gor Mahia kutokana na majina yao kuchelewa kuwasilishwa CAF.

Yanga itaondoka leo tayari kuikabili Gor Mahia katika mchezo wa mkondo wa kwanza wa Kombe la Shirikisho Afrika utakaopigwa Nairobi siku ya Jumatano, Julai 18 2018.

11 COMMENTS:

  1. HAKUNA MATUMAINI MNAENDA KUTIA AIBU TU HUKO....HILI SUALA LA KUGOMA GOMA HIVI KWANINI HALIISHI??????????

    ReplyDelete
    Replies
    1. Viongozi wababaishaji awaelezi ukweli awana umoja awakubali kuwa wameshindwa wacha tutaabike ili tujifunze

      Delete
    2. Wewe unayeweza umechangia shilingi ngapi? Ningewaona wa maana mngekuwa mnachanga pesa ili wachezaji walipwe mishahara vinginevyo kaa kimya wacha viongozi wafanye kwa uwezo wao

      Delete
  2. da!xijuiitakuaje but hii ni aibu kubwa xana kila xiku migomo but no way nitazidi kuimboea timu yangu

    ReplyDelete
  3. Huu ni uzembe uliopindukia kwa viongozi.wanajua kabisa kuna mapungufu makubwa kwenye kikosi then wanachelewesha kuwasilisha majina, hawana budi kujiuzulu

    ReplyDelete
  4. This comment has been removed by the author.

    ReplyDelete
  5. HIVI YANGA MBONA MNATUAIBISHA HIVI.....MIMI NITAANDIKA BARUA TFF ILI ITOE ONYO AMA KUWAADHIBISHA VIONGOZI WA TIMU ZOTE ZINAZOSHIRIKI MASHINDANO YA KIMATAIFA, KAMA HAKUNA MAANDALIZI YA KUTOSHA , NA KUWA KAMA WACHEZAJI HAWAPEWI MAANDALIZI MAZURI, MAZOEZINI, MALIPO NA MOTISHA NZURI, SAFARINI KUKOSA WACHEZAJI MUHIMU, MWISHONI KATIKA MECHI AMBAPO WANAWAKILISHA NCHI NA KUBEBA BENDERA YA NCHI.....MWISHONI KUISHIA KUFUNGWA AIBU SIO KWA YANGA TU BALI TAIFA ZIMA...RAISI MAGUFULI NAKUMBUKA ALISEMA IFIKE MWISHO TIMU ZETU ZISIWE ZINAISHIA KUFUNGWA FUNGWA TU, NI AIBU SANA...IFIKE MWISHO SASA. YANGA HAWAKUSHIRIKI CECAFA WAKISEMA WACHEZAJI WAO HAWANA MIKATABA, NA WAMEPEWA RUHUSA YA KUPUMZIKA, SASA CAF IMEFIKA NAPO BADO KUMBE HATA MIKATABA HAWAJAPEWA NA WENGINE WANAGOMA, MAJINA YA WACHEZAJI WATATU YAMECHELEWA CAF, HAYA BADO USAJILI UNASUASUA HUU NI UPUUZI MKUBWA....HAIVUMILIKI LAZIMA VIONGOZI WOTE WAJIUZULU.....TUNAKWENDA KUIAIBISHA NCHI...KUNA HAJA GANI YA YANGA KUSHIRIKI MASHINDANO HAYA IKIWA KWAMBA WANAENDA KUPELEKA KIKOSI KISICHO IMARA...WATANZANIA IMEFIKA WAKATI TUSIWE TUNATEGEMEA MIUJIZA, AU BAHATI...MPIRA NI SAYANSI NA MAANDALIZI, NA MOTISHA KWA WACHEZAJI NA BENCHI LA UFUNDI.....USANII NA USWAHILI SWAHILI UFIKE MWISHO....WAPENZI WA SOKA TANZANIA TUMECHOKA KUWA WASINDIKIZAJI NA KICHWA CHA MWENDAWAZIMU JAMANI......

    ReplyDelete
  6. Acha tupambane na hali ze2 haya yote n mapito

    ReplyDelete
  7. Acha tupambane na hali ze2 haya yote n mapito

    ReplyDelete
  8. KUNA KUNDI KUBWA LA WANACHAMA NA MASHABIKI WA YANGA WAMEPANGA KUFANYA TUKIO LA MASHAMBULIZI KWA WOTE WANAOHUSIKA NA KUIDHOOFISHA YANGA KWENYE USAJILI KUNDI HILO LITAFANYA VURUGU HIZO MUDA WOWOTE....WAMESIKIA MENGINE YA UCHUNGU IKIWAMO KOCHA MWINYI ZAHERA KUTOKUWA NA KIBALI MPAKA LEO HII, KELVIN YONDANI ANASAINI SIMBA JIONI HI I NA MENGINE....SASA USALAMA WA VIONGOZI WA YANGA MASHAKANI, AKIWAMO MANJI AMBAYE NAYE AMEGUNDULIKA KUWA KUSUASUA KWAKE KUINGILIA KATI KUNAWAWEKA WAO KATIKA SINTOFAHAMU...HABARI NDIYO HIYO!

    ReplyDelete

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic