July 9, 2018


Klabu ya soka ya Yanga kupitia uongozi wa matawi yake nchini umelitaka Shirikisho la Soka Tanzania kuwapatia fedha zao ambazo ni zawadi ya mshindi wa tatu katika Ligi kuu Bara.

Kwa mujibu wa Katibu Mkuu wa matawi Yanga nchini, Boaz Ikupilika, amesema kuwa TFF inawapaswa kuwapatia fedha zao hizo ambazo halali hao baada ya kumaliza wakiwa nafasi ya tatu katika msimu wa 2017/18 uliomalizika hivi karibuni.

Ikupilika ameeleza suala la wao kuzizuia fedha hizo si sahihi maana ni haki yao kupewa ili zitumike ndani ya klabu na haswa kipindi hiki Yanga ipo kwenye wakati mgumu kiuchumi.

Ikumbukwe Yanga ipo kambini hivi sasa ikijiandaa na mashindano ya Kombe la Shirikisho ambapo Julai 18 2018 itakuwa ina kibarua dhidi ya Gor Mahia FC ya Kenya.

Tayari kikosi cha timu hiyo kimekuwa kikiendelea kujifua kwenye Uwanja wa Chuo cha Polisi Kurasini tayari kukipiga na Gor Mahia kwenye mchezo wa mkondo wa kwanza huko Kenya.

3 COMMENTS:

  1. HII NI RAHISI SANA.....USHAURI, ANDIKENI BARUA CAF KUELEZA MALALAMIKO YENU AMBAYO NI YA MSINGI. KUHUSU VIFAA VYA MASHINDANO YA CAF. NA PESA YA MATAYARISHO YA MICHEZO YA GROUP STAGES, NA PESA ZENU ZA UBINGWA MUWAANDIKIE VODACOM ILI TFF WAAIBIKE, COPY ZA BARUA ZIENDE, BMT, WAZIRI WA MICHEZO, CAF AND FIFA

    ReplyDelete
  2. UKAGUZI WA MAPATO NA MATUMIZI, PIA KUHAKIKI UHALALI WA MADENI UFANYWE KATIKA TAASISI ZIFUATAZO
    1. BODI YA LIGI YA TFF NA VODACOM
    2. TFF
    3. YANGA KUHUSU MATUMIZI NA MAPATO YA USHIRIKI WA MASHINDANO YA CAF MWAKA HUU

    UKWELI UANIKWE KWENYE VYOMBO VYA HABARI....ILI MBIVU NA MBICHI ZIJULIKANE!!

    ReplyDelete
  3. Lakini sifikiri kuanzia sasa na kuendelea kama kutakuwa na shida ya pesa kwa yanga kwa kuwa imeshatangazwa kuwa time yoyote Manji atarejea kwa kishindo kwakuwa ombi lake la kujiuzulu limekataliwaa na hapa inaonesha kuna heri kubwa ambayo itajaalia tuyasahau machungu na huku wanaoitakiya maovu yanga wasiweze kunyanyua nyuso zao

    ReplyDelete

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic