July 9, 2018


Katibu Mkuu wa Baraza la Wazee Simba, Felix Makua, ameibuka tena na kuutaka uongozi wa klabu hiyo kuanza mchakato wa kufanya uchaguzi haraka.

Kwa mujibu wa Radio One, Makua amefunguka na kusema mpaka sasa uongozi wa Simba umekuwa kimya bila kujua kama muda uchaguzi mkuu unaopaswa kuchagua viongozi watakaoiongoza Simba kwa miaka minne ijayo umefika.

Katibu huyo ameeleza kuwa Makamu Rais wa Simba, Salim Abdallah 'Try Again' amekuwa akiwaambia wanachama kuwa klabu ipo kwenye mchakato wa kukamilisha mabadiliko ya katiba wakati ni kitu ambacho si sahihi.

Makua ameeleza kuwa Simba inaitambua katiba ambayo ilipitishwa mwaka 2014 akieleza inatambulika mpaka katika Shirikisho la Soka Tanzania (TFF) hivyo akiombe ni vema ikafuatwa.

Ikumbukwe utawala wa awamu ya hii uliopo madarakani unamaliza muda wake mwishoni mwa mwezi huu ambapo katiba mpya ya Simba ipo kwa Msajili wa serikali kwa ajili ya kukamilishiwa mabadiliko ya kuupokea rasmi mfumo mpya wa mabadiliko ndani ya Simba.
2 COMMENTS:

  1. Mbona kiblog chakoo kishaanzaa uchokooooo....unahangaikaa na vizeee vinavyokwamisha sokaaa vyann??? G jifunziii kwa wenzioooo....ndo mana soka la tz halisongi sijui hujifunzi yanga wanavyo tesekaaa... Kiblog kishaanza kuwa cha uboya

    ReplyDelete
  2. Kiblog hakipo kuhamasisha maendeleo ya mpira bali uzushi uhasidi nä majungu. Kila mahali kinatafuta uchochezi na majungu. Hai wanaodai ni wazee hata uchaguzi ukifanyika hawatahudhuria.Mikutano imefanyika hawajashiriki bali wanakaa pembeni na kupewa publicity nä bi blog uchwara vikiongozwa na blog hii. Ni wakati muafaka wanasimba na viongozi tukaisusa hii blog .Haji Manara kama msemaji toa mwongozo.

    ReplyDelete

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV