Katibu wa Baraza la Wazee la Yanga, Ibrahim Akilimali, amewataka mashabiki na wanachama wa Yanga kutokukubali kuchanga pesa zao kwa kuwa anaamini hazitokuwa katika sehemu salama.
Akilimali ametoa kauli hiyo ikiwa ni baada ya hivi karibuni klabu hiyo kutangaza mpango huo wa kuchangiwa na wanachama na mashabiki wa timu hiyo ya Jangwani.
Ikumbukwe pia, msimu uliopita Yanga SC ilianzisha mfumo huo wa kuomba michango kwa wanachama lakini hawakuwaeleza kuwa walipata shilingi ngapi.
Mzee Akilimali alisisitiza kuwa si vyema kwa Yanga kuendeshwa kwa mfumo huo na badala yake viongozi waliopo madarakani kujiuzulu ili kufanya mabadiliko ya kiuongozi ambayo anaamini ndiyo suluhisho ya hayo yote.
“Nawaomba wana Yanga hasa wenye uchungu na kuipenda timu yao wasitoe hata senti moja kwa sababu hakuna usalama wa kile kitakachotolewa, nasema haya kwa akili sana na kwa uchungu sana.
“Ni bora viongozi walioko madarakani sasa wajiuzulu wote na kuipisha Yanga iingie katika uchaguzi wa viongozi wapya ambao mfumo huo wa kisasa umekuwa ukitumika na Yanga tangu mwaka 2008, hilo ndilo litakuwa suluhisho,” alisema Mzee Akilimali.
CHANZO: CHAMPIONI
Huyu Mzee naye hamnazo kweli, Club imepewa siku 75 kufanya uchaguzi sasa wakijiuzuru timu itaendeshwaje? Ameichangia nini Yanga amebaki kupiga domo tu>
ReplyDeleteAnaitwa Mzee Domokaya bin Mchumia Tumbo. Aliposema Manji ukiondoka ataleta mwekezaji huyo mwekezaji wake yuko wapi mpaka leo? Hii inaonesha hana uchungu na timu au anadhani timu inaendeshwa kwa nguvu za jua. Kambi iliyowekwa Morogoro wachezaji na benchi wanakula hewa!! Kosa mali upate akili. Ama manju wa kiswahili Mzee Shaaban Robert alipata kusema "UTU BUSARA, UJINGA HASARA!"
ReplyDelete