August 30, 2018


Na George Mganga

Baada ya kupoteza mchezo wa kukamilisha ratiba jana dhidi ya Rayon Sports katika mchezo wa Kombe la Shirikisho Afrika kwa kufungwa bao 1-0, Mratibu wa timu hiyo, Hafidh Saleh, amesema kazi rasmi wanakuja kuanza Ligi Kuu.

Saleh ameeleza hayo kutokana na kiwango safi ambacho walikionesha kwa kuwa na asilimia kubwa ya umiliki wa mpira dhidi ya wapinzani wao.

Kiongozi huyo ameeleza kwa sasa nguvu zao zote zinakuja kufanya kazi katika Ligi Kuu Bara ambapo ratiba ijayo inaonesha mechi yao ijayo itakuwa dhidi ya Mwadui FC.

Baada ya kupoteza jana na kushindwa kusonga mbeke, Yanga inatarajiwa kuwasili jijini Dar es Salaam leo tayari kuanza maandalizi ya mechi za ligi.

Katia kundi D ambalo Yanga ipo, timu za USM Alger na Rayon Sports zimefanikiwa kuingia hatua inayofuata huku Gor Mahia na Yanga zikiondoshwa.

2 COMMENTS:

  1. Tuliyeni mjithamini kwanza. Kipindi cha pili mlipotea kabisa. Jitayarisheni kwanza kabla vitisho visivyo uzito. Huyo mlookuwa munamuamini kwa kila kitu si alitolewa baada ya dakika sitini za mchezo.

    ReplyDelete
  2. Tena mmcheza na Rayon ikiwa na pengo la wachezaji 9 wa timu ya kwanza.First eleven kutokana na wachezaji wao kufungiwa na CAF baada ya vurugu kwenye mechi iliyopita na timu kutoka Algeria .Wengine wamegoma kwa mikataba kwisha.Mngecheza nä Rsyon kamili kipigo kingekuwa mkubwa zaidi.

    ReplyDelete

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic