August 30, 2018


Mwenyekiti wa Chama cha Kutetea Haki za Wachezaji (SPUTANZA), Mussa Kisoki, amepingana na maamuzi ya TFF kuwatema wachezaji sita wa Simba kwenye kikosi cha Taifa Stars.

Kisoki amesema suala la nidhamu linapaswa kuchukuliwa maamuzi ya busara badala ya kuanza kutoa huku haraka kulingana na hatua ya soka letu namna ilivyo.

Mwenyekiti huyo amesema TFF hawakupaswa kufanya hivyo ukizingatia soka la Tanzania ndiyo kwanza lipo kwenye mchakato wa kukua, hivyo kuwaondosha wachezaji hao sababu ya nidhamu ni kuiharibu Tanzania kisoka.

Kisoki ameshauri kuwa ifikir hatua TFF wajaribu kuangalia soka letu lipo hatua ipi na pia akisema ni vema wachezaji hao wangeshauriwa vizuri tu ili kuweka mambo sawa badala ya kuwondoa sababu ya kuchelewa kambini.

Katika wachezaji 7 wa Simba walioitwa, 6 waliondolewa kutokana na kuchelewa kuripoti kambini wakati kipa Aishi Manula pekee akisalia baada ya kuwahi.

12 COMMENTS:

  1. TFF HAWAKUTUMIA BUSARA HATA KIDOGO NA SASA KOCHA HUYO HATOPATA USHIRIKIANO WA MASHABIKI WA SIMBA JEE MNAJENGA TIMU AU MNABOMOA? MNAHITAJI BUSARA KWENYE KUFANYA MAAMUZI YANAYOHUSU TAIFA ZIMA SI KWA UTASHI WAKO. KOCHA ATASHINDWA KUFANYA KAZI YAKE KAMA ANAANZA KUJA KWA KIDIKTETA. AELEWE TIMU YA TAIFA NI YETU WOTE. KLABU NDIO INANUNUA WACHEZAJI, INAWAGHARAMIA, INAWALIPA MISHAHARA NA HATA WAKIUMIA KWENYE TIMU YA TAIFA KLABU NDIZO ZINAWAGHARAMIA MATIBABU YAO BASI PAWEPO NA KUHESHIMIANA KATI YA KOCHA, TFF NA KLABU NA WACHEZAJI. HAWA SIO WATOTO WA SKULI NI WATU WAZIMA WENYE FAMILIA. ACHENI KUNYANYASA WACHEZAJI. WACHEZAJI WANA HAKI ZAO PIA. SAMATA AMESHARIPOTI? MBONA HAMUMUONDOWI?

    ReplyDelete
  2. Enter your comment...mie naona Tff watakuwa wanataka kulipolomoa soka la Tanzania kwa sababu taifa letu halijafikia huko pia bado kishelia mchezaji anatakiwa alipoti kambini saa 72 kabla ya mchezo nikutokana na ratiba ya kilabu husika anyway tuyaache maana tumeshakuwa na maprofesion wa kisoka tuombe ishinde isipo shinda yatamkuta ya Caro's Dunga kumuacha Ronadinho.

    ReplyDelete
  3. Replies
    1. Jina lenyewe lina F mbili.. Hizo busara ndo watakuwa nazo sasa..??
      Ila itakuwa wana njama za kuinufaisha Uganda Cranes.
      Si bure!

      Delete
  4. Wachezaji sio watoto wa skuli.TFF mnaanzisha mgogoro na klabu na inaonyesha mmeshaanza kutafuta kafara mapema

    ReplyDelete
  5. Washabiki hewa utawajua tu,ni upuuzi kupingana na TFF,hata mchezaji awe mzuri vipi asipokuwa na nidhamu ni kazi bure,msiingize uteam kwenye suala la maendeleo.Lazima kila mtu aheshimu mamlaka.

    ReplyDelete
  6. Huyo Kisoki nae hewa tu sababu alizotoa hazina mashiko,hao sio watoto useme wapewe muda,kujiona mapro ndo shida ilipo next time wakiitwa watazingatia

    ReplyDelete
  7. Kanuni zinaonyesha saa 48 kabla ya mchezo husika.Huwezi kulazimisha kanuni kwa sababu kocha kataka hivyo .Kujenga ni magumu lakini kubomoa ni rahisi sana.

    ReplyDelete
  8. Kwani kanuni zinataka wachezaji waripoti kabla ya siku ngapi kabla ya mechi? Mbona tff mnatuchanganya?

    ReplyDelete
  9. Wachezaji hao hata pindi wakirejeshwa hawatakuwa na morali au kumpenda kocha huyo tena kwani wachezaji hao ni wenye heshima zao na wapendwa wakuu na mashabiki na bila ya shaka wanahisi kuwa ilikuwa ni mipango kuwaharibia maisha yao ya kimaisha na ya kimchezo. Si tumeona jinsi wachezaji wa Azam nyota pale walipopuuzwa na jinsi walivonyangnyiwa na kuwa nyota wakuu huko walipokwenda

    ReplyDelete

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic