August 30, 2018


Na George Mganga

Baada ya kutangaza kuwatema wachezaji sita wa kllabu ya Simba waliokuwa wameitwa katika kikosi cha Taida Stars, Katibu Mkuu wa Shirikisho la Soka Tanzania (TFF), Wilfred Kidao, amesema hakuna aliye juu ya timu hiyo.

Kidao ameeleza kuwa ukubwa au umaarufu wa jina la mchezaji kupitia klabu yake, haimaanishi kuwa kutakuwa na busara ambayo itaweza kutumika haswa kwa TFF hii ambayo ipo chini ya Wallace Karia.

Katibu huyo amesema Stars inapaswa kupewa heshima yake na nidhamu kuwekwa mbele na ndiyo maana wameamua kuwaondoa wachezaji hao ambao waliitwa kwa ajili ya kujiandaa na mchezo wa kuelekea kufuzu AFCON dhidi ya Uganda, Septemba 8 2018.

Kiongozi huyo amesisitiza kwa kusema nidhamu kwanza ndiyo inapaswa kuwekwa mbele na bila kufuatwa hawatakuwa na cha msalia mtumu kwa kipindi hiki.

Wachezaji walioondolewa ni Nadhodha John Bocco, Shiza kichuya, Jonas Mkude, Erasto Nyoni, Shomari Kapombe pamoja na Hassan Dilunga.

Kwa upande wa viongozi wa Simba ambao ni Meneja wa Klabu, Richard Robert ,pamoja na Kaimu Katibu Mkuu, Hamis Kisiwa, Shirikisho la Mpira wa Miguu nchini (TFF) kwa kufuata kanuni limewapeleka kwenye Kamati ya Maadili kwa kutotimiza wajibu wao.


Baada ya kuondolewa, wachezaji walioitwa kuchukua nafasi zao ni Paul Ngalema wa Lipuli FC, Salumu Kimenya wa Tanzania Prisons, David Mwantika na Frank Domayo wa Azam FC, Salumu Kihimbwa na Kelvin Sabato wa Mtibwa Sugar na Ali Abdulkadir.


4 COMMENTS:

  1. HUNA BUSARA SUALA LA KUZUNGUMZA NA WACHEZAJI NA KLABU HUSIKA LINAKUSHINDAJE

    ReplyDelete
  2. Sio shida ninacho jua mnataka kuhongwa kwani kuna umuhimu gani kuchezea taifa wakati hata mchezaji akiumia amumpi mahitaji

    ReplyDelete
  3. Nyie msijenge vurugeni tu.
    uma umeshapoteza imani na inahitaji hatuwa za haraka kuzuwia mporomoko na kuweka sawa mambo ambapo naamini si rahisi. Eenye busara waingie kati haraka mambo hayabashiri kheri kila kona zinalalamika. Ratiba kuuliwa kabla ya kuzaliwa kuzitia hasara timu ambazo taabani kipesa

    ReplyDelete
  4. Nina hakika wengi wataishangilia Uganda kutokana na ghadhabu ambayo wamechukizwa na vitendo vya kocha a TFF kumkubalia huyo kocha kwa kukiangusha kikosi cha taifa

    ReplyDelete

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic