August 30, 2018


Na George Mganga

Baada ya kutangazwa wachezaji sita wa Simba kutemwa ndani ya kikosi cha timu ya taifa, Taifa Stars, mashabiki wengi wa klabu hiyo wamoneshwa kuchukizwa na maamuzi ya Shirikisho la Soka Tanzania (TFF).

Jana kunako Makao Makuu ya Shirikisho hilo lililopo mitaa ya Karume, Ilala, Dar es Salaam, Kocha Mkuu wa Stars kupitia Katibu Mkuu wa TFF, Wilfred Kidao, alitangaza kuwaondoa wachezaji 6 wa Simba huku akiachwa Kipa Aishi Manula pekee.

Kutokana na maamuzi hayo, asilimia kubwa ya mashabiki wengi wa Simba wamefunguka kuwa kueleza kuchukizwa zaidi na maamuzi hayo huku wakifikia hatua ya kusema hawatainga mkono Stars itakapocheza na Uganda.

Sababu za kuwaondoa wachezaji hao ni kutokana na kuchelewa kuripoti kambini kwa ajili ya kuweka kambi maalum tayari kuanza maandalizi ya kucheza na Uganda.

Mbali na kutoiunga mkono Stars, mashabiki wameeleza kufuata nyayo za nyota wao, Emmanuel Okwi wakiahidi kuishabikia timu ya Uganda ambayo watacheza nayo Septemba 8 katika mchezo wa kuelekea kufuzu AFCON huko Kampala Uganda.

Aidha, wengi wao wameleeza kushangazwa na maamuzi hayo ya TFF wakisema wamefeli huku wakishauri kuwa ilipaswa suala la nidhamu liende polepole.

Wachezaji wa Simba waliondolewa ni Nadhodha John Bocco, Shiza kichuya, Jonas Mkude, Erasto Nyoni, Shomari Kapombe pamoja na Hassan Dilunga.

13 COMMENTS:

  1. TFF WAMEYATAKA NA SASA KOCHA HUYO HATOPATA USHIRIKIANO WA MASHABIKI WA SIMBA JEE MNAJENGA TIMU AU MNABOMOA? MNAHITAJI BUSARA KWENYE KUFANYA MAAMUZI YANAYOHUSU TAIFA ZIMA SI KWA UTASHI WAKO. KOCHA ATASHINDWA KUFANYA KAZI YAKE KAMA ANAANZA KUJA KWA KIDIKTETA. AELEWE TIMU YA TAIFA NI YETU WOTE. KLABU NDIO INANUNUA WACHEZAJI, INAWAGHARAMIA, INAWALIPA MISHAHARA NA HATA WAKIUMIA KWENYE TIMU YA TAIFA KLABU NDIZO ZINAWAGHARAMIA MATIBABU YAO BASI PAWEPO NA KUHESHIMIANA KATI YA KOCHA, TFF NA KLABU NA WACHEZAJI. HAWA SIO WATOTO WA SKULI NI WATU WAZIMA WENYE FAMILIA. ACHENI KUNYANYASA WACHEZAJI.

    ReplyDelete
    Replies
    1. NEW COACH GO HOME THIS DECISION IS UNFAIR TO OUR PLAYERS

      Delete
  2. HAPO TFF WAMECHEMSHA WALUDI TENA MEZANI

    ReplyDelete
  3. Soka la Tanzania haliwezi kupiga hatua kwa kufanya mambo kwa mazoea, Taifa stars ni ya watanzania wote siyo hao takataka simba wanaojiona wafalme wakati viwango vyenyewe zero. Nafurahi kwa msimamo wa kocha maana Tanzania tumekuwa tukiwaabudu sana wachezaji wa simba na yanga wakati kuna wengine kibao wenye uwezo hata kuwazidi hao. Pig up team coach

    ReplyDelete
    Replies
    1. takataka mama yako mzazi fala ww

      Delete
    2. Ushabiki usio na tija unalimaliza soka nchi hii. Hakuna mchezaji mkubwa kwa timu ya Taifa. Taifa ni kubwa kuliko wachezaji. Mashabiki maandazi kwanini hawajiulizi Mbwana Samata kwanini huwa hachelewi kujiunga na timu akiitwa? Je yeye na hao wachelewaji masupa star nani super star? Tukitaka soka letu likue tutazame nidhamu kwanza povu halitasaidia. TUBADILIKE

      Delete
  4. Hakuna soka bila nidhamu. NA WANAOSHABIKIA UKOSEFU WA NIDHAMU WATAPATA MAJAWABU YAKE.

    ReplyDelete
    Replies
    1. Ebu toa maana ya nidhamu katika kadhia hii!
      Je wachezaji (WOTE - kazia wote) walitakiwa kuripoti kambini mwisho lini..?
      Wachezaji wa hiyo timu moja wamechelewa kwa muda gani ulioathiri mazoezi ya hiyo timu ya tajwa?
      Je walioitwa kuchukua nafasi zao ndo wameyawahi hayo mazoezi kuliko walioitwa awali..??
      Je vipi kuhusu wa timu nyingine ambao bado hawajaripoti kambini..??

      Daima ukitaka kufanya maamuzi ya busara na ya kujenga usikurupuke..!!
      TFF ikiri tu kuwa imekurupuka na inajitahidi kuiandalia Uganda Cranes ushindi wa kishindo!

      Delete
  5. Hatukatai nidham ni muhimu kila mahali lakini ameharakisha mno.angewapa onyo kwanza

    ReplyDelete
  6. Wisdom rather than anger desperately needed to protect these elite players that billions were spent to bring them where they are now. It should well be understood, such problems are not rare in the world of soccer. It is the obligation of the TFF to repair rather than accept destruction. A dirty hand is not amputated, but it is washed with soap and perfume. A good teacher doesn't expell stubborn pupils because he is there to lead his pupils to achive parents' hope. TFF should not easily support a situation that could eventually destroy what we have achieved after long years of hard work and patience. Such players are badly needed elsewhere and we should not easily open the doors for others to benefit after our long years of preperation because immediate replacement is ompossible. A coach is a humanbeing who needs advice

    ReplyDelete
  7. Kocha Amonika kachaguwa uadui na Wanasimba badala ya kuchaguwaapenzi na maelewano. Kajitengenezea ubaya kwa wachezaji huku akiungwa mkono TFF jambo ambalo wengi hawatomtakia mafanikio kocha huyo na kuiweka timu ipoteze moral haya ilibidi wakoo wa TFF wayajuwe mapema. TFF ilianza vizuri lakimi sasa inapoteza imani. Inabidi wajirekebishe mapema kabla meli kwenda mrama

    ReplyDelete
  8. Timu bora ya Taifa ni ushirikiano kati ya vilabu na shirikisho. Huu utaratibu wa kuifanya timu ya Taifa kama kilabu ndio unaleta shida. Sharia ni masaa 72 kabla ya mchezo nyie mnataka wiki mbili kabla jipimeni. Mmefeli kutafuta wadhamini kuendesha ligi mnategemea timu ipi bora ya Taifa

    ReplyDelete

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic