DIAMOND, WCB WAMUOMBEA OMMY DIMPOZ KWA MUNGU
Staa wa Bongo Fleva, Diamond Platnumz ameweka pembeni tofauti zilizokuwepo kati yake na Ommy Dimpoz katika wakati huu ambapo Dimpoz ni mgonjwa na kumuombea kwa Mungu apone mapema ili aweze kurudi katika hali yake ya kawaida na kuendeleza game ya muziki.
Kupitia ukurasa wake wa Instagram, Diamond amepost picha ya Dimpoz na kumuombea apone huku meneja wake, Babutale na msanii rayvanny nao wakifanya vivyo hivyo.
Diamond Platinumz; “Inshaallah! Mwenyezi Mungu akufanyie wepesi, uweze pona haraka na Kurudi kuendelea na sanaa ili pamoja tuzidi peleka Mziki wetu Mbali zaidi…
Babu Tale; “Get well soon bro Mungu akutie nguvu upone urudi kwenye hali yako ya kawaida @ommydimpoz.”
Ray Vanny; “Mungu Akusimamie katika kipindi hiki… upone na Urudi katika afya Yako…. Get well Soon Brother”
Nay wa Mitego; Get Well Soon Brother @ommydimpoz Mungu Akupe Afya Kama Zamani Urudi Kwenye Kazi Zako Ukiwa Fit. Tunakuombea🙏🏿🙏🏿”
Madee; “Kwenye maombi yetu yakila siku tusimsahau Omary.. … tumuombee apone haraka aendelee na majukumu yake, Omary anaumwa”.
Ni mwezi wa tatu sasa tangu Ommy Dimpoz atangaze kuwa amefanyiwa upasuaji wa koo, licha ya kwamba hakuna taarifa rasmi zilizotolewa na uongozi wake juu ya maendeleo ya afya yake na jana alirudishwa nchini Afrika Kusini kwa matibabu baada ya hali yake kuendelea kutokuwa vizuri.
Aidha, uongozi wa Rockstar 4000 umesema taarifa zilizosambaa katika mitandao ya kijamii kuwa msanii, Omary Nyembo maarufu Ommy Dimpoz kuwa amelazwa hospitali katika chumba cha uangalizi maalum (ICU) hazina ukweli wowote.
0 COMMENTS:
Post a Comment