August 31, 2018


Na George Mganga

Kocha wa Dodoma FC, Jamhuri Kihwelo 'Julio', amepingana na aliyekuwa Mwenyekiti wa zamani wa klabu ya Simba, Ismail Aden Rage, kuhusiana na kuondolewa kwa wachezaji 6 Simba ambao waliitwa Taifa Stars.

Julio ameeleza kuwa sababu alizozitaja Rage kuwa Kocha Mkuu wa Taifa Stars, Emmanuel Amunike alipaswa kuwapa onyo wachezaji hao si sahihi kwani ni kuendelea kulea uozo wa soka la Tanzania.

Julio amepingana na Rage kwa kusema ifikie hatua Taifa Stars ipewe heshima yake na ni vema suala la nidhamu liwekewe msisitizo zaidi ili kuwanyoosha wachezaji ambao wamekuwa mzigo.

Rage ambaye aliwahi kuiongoza Simba, alisema Amunike alipaswa kuwapa onyo wachezaji hao badala ya kuwaondoa au kuwapiga walau faini ili kuweka mambo sawa.

Mawazo ya Rage yamesababisha kumuibua Julio na kusema kwa utatribu huo safari ya kukuza soka la Tanzania bado itakuwa ngumu.

Stars imeanza kambi jana tayari kuanza maandalizi ya mchezo wa kuelekea kufuzu AFCON dhidi ya Uganda ambapo mchezo utapigwa Septemba 1 huko Kampala.

2 COMMENTS:

  1. Hao wanaofurahia kuondoshwa kwa wachezaji wa Simba Timu ya Taifa wasije kuja kuwa wa kwanza kuwasema kwa ubaya wachezaji hao pindi Taifa Stars kwa bahati mbaya ikaja kuboronga mbele ya safari. Kwa wale wachezaji waliondolewa Taifa Stars wala hawapaswi kabisa kulifikiria suala hilo kwani linaweza kuwatoa mchezoni cha kufanya ni kufokasi na timu yao ya Simba na wawe tayari kuipigania mpaka tone la damu la mwisho kwani ndipo kazi zao zinapothamniniwa zaidi. Ni vitu vya hovyo kabisa kwani ukiliangalia suala hili tayari limeshaingia katika siasa za yanga na Simba. Wanazi wa Yanga makalio yapo wazi kwa furaha kisa wachezaji wa Simba hawamo Taifa Stars. Ukienda kuangalia Msahafu wa FIFA unasemaje juu ya wachezaji muda gani anatakiwa kujiunga na timu ya Taifa basi utagundua yakwamba mpira wetu unaongaozwa na watu wa maigizo.

    ReplyDelete
  2. Huyu mzee ni kuma ndo maana anahangaika na timu za mtaani pyuuuuuuuuu!

    ReplyDelete

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic