August 31, 2018


Wakati Shirikisho la Soka Tanzania likiwa tayari limeshatoa siku 75 ambazo sasa zinazidi kuelekea ukingoni kwa ajili ya klabu za Simba na Yanga kufanya uchaguzi, Katibu Mkuu wa Matawi ya Yanga, Boza Kupilika, amesema wao wanamtambua Yusuf Manji kuwa ni Mwenyekiti wao.

Kupilika amefunguka hayo kutokana na TFF hivi karibuni kuwataka Yanga wafanye uchaguzi mkuu badala ya kujaza nafasi pekee za viongozi waliojiuzulu.

Katibu huyo amesema kupitia Mkutano Mkuu wa Yanga uliofanyika mnamo Juni 10 2018 kwa pamoja wanachama wa klabu hiyo waliadhimia Manji kuendelea kuwa Mwenyekiti wa klabu.

Wanachama hao walifikia mwafaka huo kwa kupinga barua ya Manji ambayo alituma akiomba kuachia ngazi Yanga kwa madai ya kwenda mapumziko na kuwa na matatizo mengine ambayo yasingeweza kumruhusu kuendelea na majukumu.

Kutokana na kuendelea na msimamo huo, Boaz pamoja na matawi yote wameamua kuusimamia na kuwataka TFF waache kuwabadilishia maamuzi hayo kwa maana ya kufanya uchaguzi wa Mwenyekiti wakati wanamtambua.

Mpaka sasa Yanga imekuwa haina Mwenyekiti kwa takribani mwaka mmoja huku pia Wajumbe kadhaa wa Kamati ya Utendaji wakijiuzulu siku zilizopita hivi karibuni.


1 COMMENTS:

  1. TFF IMESHASEMA YANGA FANYENI UCHAGUZI> HAWA TFF HAWANA DHAMANA NA MTU WAMEWAONEA NA KUWATIMUA WACHEZAJI 6 WA SIMBA NA 1 WA YANGA KUTOKA TIMU YA TAIFA BILA KUJALI MADHARA YAKE. SIKU 75 ZINAPITA TFF WASIJE WAKAWAFUNGIA YANGA KUCHEZA LIGI MAANA TFF WAMEKOSA MFADHILI WA LIGI KUU WA MAANA SASA WATATAFUTA WAKUMSHUSHIA KIPIGO. SOKA LETU BANA

    ReplyDelete

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic