August 31, 2018


Uongozi wa Yanga kupitia kwa Matawi ya klabu hiyo umeibuka na kusema utamtumia barua Waziri wa Habari, Sanaa, Utamaduni na Michezo inayoeleza kuwa mpaka sasa wanamtambua Yusuf Manji kuwa Mwenyekiti wao.

Hatua hiyo imekuja mara baada ya Shirikisho la Soka nchini (TFF) kuwataka Yanga kufanya uchaguzi mkuu baada ya aliyekuwa Mwenyekiti wao, Manji kutangaza kuachia ngazi takribani mwaka mmoja na miezi kadhaa iliyopita.

Kwa mujibu wa Katibu Mkuu wa Matawi, Boaz Kupilika, amesema wanajipanga kuandika barua hiyo ili iweze kumfikia Mwakyembe haraka.

Aidha, Kupikika amesema barua hiyo itaeleza kumtaka Waziri huyo kuwazuia Yanga awanyime mamlaka TFF ya kuwataka wafanye uchaguzi huo kwasababu wanatambua Manji kuwa bado ni Mwenyekiti wa klabu.

Hivi karibuni TFF ilitoa siku 75 kwa klabu za Simba na Yanga kuzitaka zifanye chaguzi ili kuwapata viongozi wengine ambao wataendelea kutawala kwa mujibu wa katiba zao.

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic