August 31, 2018


Na George Mganga

Shirikisho la Soka nchini (TFF) eo linakutana na uongozi wa klabu ya Simba kunako makao makuu yaliyopo mitaa ya Karume, Ilala, Dar es Salaam.

TFF wanakutana na Simba kwa lengo la kuweza wazi sakata la kuondolewa kwa wachezaji wake 6 ambao walikuwa wameitwa kwenye kikosi cha timu ya taifa, Taifa Stars.

Uongozi wa shirikisho hilo utaweza wazi juu ya suala hilo sambamba na Simba wenyejewe juu ya wachezaji hao ambao wamekuwa gumzo kubwa kwenye vyombo vya habari.

Wachezaji wa Simba waliondolewa kwenye kikosi na Kocha Mkuu, Emmanuel Amunike kwa kuchelewa kuripoti kambini huku Kipa Aishi Manula pekee akiwahi.

Wachezaji ambao waliondolewa ni Shiza Kichuya, Shomary Kapombe, Jonas Mkude, Hassan Dilunga, John Bocco na Erasto Nyoni.

Idaidi ya wachezaji walipaswa kuanza mazoezi na wenzao jana kwenye Uwanja wa Bocco Veterani tayari kujiandaa na mchezo wakufuzu kuelekea AFCON dhidi ya Uganda, Septemba 8 2018 huko Kampala.

5 COMMENTS:

  1. HAPAKUWA NA SABABU YA KUKUTANA WAKATI TFF TAYARI WAMETOA ADHABU KWA WACHEZAJI NA VIONGOZI 2 WA SIMBA. TFF WANACHOKIHITAJI NI MLANGO WA KUTOKEA KUTOKANA NA LAWAMA WANAZOZIPATA WANATAKA SIMBA WAOMBE RADHI LAKINI HAKUNA HAJA MBONA TAYARI WACHEZAJI WENGINE WAZURI WAMESHATEULIWA.

    ReplyDelete
  2. TFF INAUHARIBU MPIRA WA NCHI YETU. KAMA NI HUYU KOCHA BASI AMEANZA VIBAYA.

    ReplyDelete
    Replies
    1. UBABE UNA MAANA GANI? TFF NA KOCHA SOMENI KANUNI ZA FIFA MZIELEWE VIZURI MMEWAONEA TU HAO WACHEZAJI.

      Delete
  3. Ivo kweki yupo beki meenye uwezo wa Kapombe, kiungo meenye uwezo wa Mkude na winga meenye uwezo wa Kichuya? Lililokuwepo sasa ni kuuwa vipaje, umiza mchezaji nyota mumtupe nje halafu mumrejeshe tena basda ya kugharamiwa matibabu na timu yake

    ReplyDelete
  4. Hao ni mara ya kwanza kucheza Stars ?Je wamefanya nini? Hakuna kubembelezana waachwe. Sababu ya kubembelezana ndicho yanatokea kama inavyotokea kwa Yanga mechi muhimu mtu achezi timu inaharibikiwa baadae anarudishwa. Timulia mbali .Amunike ni kocha mkubwa sana kwa wachezaji wetu hawajafika hata robo ya mafanikio yake

    ReplyDelete

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic