August 14, 2018


Baada ya kuambulia kichapo kutoka kwa Alliance ya Mwanza na kwenda sare dhidi ya Singida United, Kocha Mkuu wa Kagera Sugar, Mecky Maxime, amefunguka juu ya madhaifu kikosini mwake.

Maxime ameeleza bado kuna mapungufu kadhaa katika safu zote za kikosi haswa ya ushambuliaji ambayo imekuwa ikishindwa kutumia nafasi zake kiuadilifu.

Kocha amesema kwa sasa atazidi kuwafua zaidi na kurekebisha makosa kadhaa ambayo yamekuwa yakijitokeza ili kabla ya pazia ligi kuu kuanza waweze kuwa fiti.

Kukosa ushindi kati ya mechi mbili tajwa hapo juu zinazidi kumpa wakati mgumu Maxime ndani ya kikosi chake na sasa ameahidi kupambana kutatua mapungufu hayo.

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic