August 14, 2018


Wakati kikosi cha Simba kikiwa jijini Arusha kujiandaa na mchezo wa kirafiki kesho dhidi ya Arusha United, uongozi wa klabu hiyo umesema hali ya mshambuliaji wake, John Bocco imeanza kuimarika.

Kwa mujibu wa Meneja wa Timu, Richard Robert, ameeleza kuwa Bocco sasa hali yake imeimarika na alikuwa sehemu ya kikosi kilichofanya mazoezi baada ya timu kurejea Dar ikitokea Lindi.

Bocco amekosekana ndani ya Uwanja katika mechi 4 mfululizo ikiwemo zile mbili za Uturuki pamoja na dhidi ya Asante Kotoko pamoja na Namungo FC.

Kutokana na hali ya mchezaji huyo kuanza kuja vizuri, kuna uwezekano mkubwa akawa sehemu ya kikosi ambacho kitacheza dhidi ya Mtibwa Sugar Agosti 18 kwenye mechi ya Ngao ya Hisani.

Bocco amekuwa akisumbuliwa na majeruhi kwa takribani mwezi mmoja na wiki kadhaa sasa kutokana na maumivu ya nyama za paja aliyopata kuelekea mwishoni mwa msimu wa Ligi Kuu Bara.

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic