August 7, 2018


Mwenyekiti wa Kamati ya Maadili Simba, Suleiman Kova, amewataka Yanga kujipanga upya ili waweze kurejea katika hali yao ya mwanzo.

Kova ambaye aliwahi kuwa Kamanda wa Kanda Maalum ya Dar es Saalam, amesema ushindani baina ya Simba na Yanga huleta chachu kubwa pale timu hizo mbili zinapokuwa zipo vizuri.

Kwa mujibu wa Radio EFM, Kova amesema hayo kutokana na mwenendo ambao walionao Yanga kwa kipindi hiki ambapo wanapitia mpito ambao unawafanya hata baadhi ya mashabiki wa timu hiyo kuvunjika moyo.

"Unajua Yanga na Simba zinapokuwa vizuri huleya upinzani na raha ya utani inakuwa safi, nawaomba watani zetu wajipange vizuri kwani hatufurahii kuoana matatizo wanayopitia yanazidi kuongezeka" alisema.

Aidha, kuelekea tamasha la Simba Day kesho Jumatano, Kova amewaomba wanachama na mashabiki wa Simba pamoja na Yanga, kujitokeza kwa wingi ili kuweza kushuhudia soka la nguvu kutoka kwa timu yao ambayo ilikuwa Uturuki kwa kambi ya wiki mbili.

Simba itashuka dimbani kumenyana na Asante Kotoko ya Ghana ambayo inawasili leo tayari kwa mchezo wa kesho.

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic