Baada ya taarifa kuelezwa kuwa Kocha Mkuu wa Singida United, Hemed Morocco kujiengua ndani ya timu hiyo, uongozi wa klabu hiyo umeibuka kivingine.
Kwa mujibu wa Mkurugenzi wa klabu ya Singida, Festo Sanga, ameibuka na kukanusha taarifa hizo akisema hazina ukweli wowote.
Hatua hiyo imekuja mara baada ya taarifa kusambaa mitanadoni zikieleza Morocco ameamua kuikacha Singida kutokana na kutotimiziwa stahiki zake muhimu ambazo awali walikubaliana.
Lakini Sanga amekanusha huku akisema Morocco bado ni Kocha wa Singida na sasa yupo Zanzibar huku akieleza baadaye atarejea kuendelea na majukumu yake ya kuinoa timu kama kawaida.
Ikumbukwe Morocco alichukua mikoba ya aliyekuwa Kocha wa timu hiyo, Mholanzi, Hans van der Plujim ambaye alitimkia Azam FC.
Morocco alianza kazi ya kuinoa Singida katika michuano ya SportPesa Super CUP iliyokuwa ikifanyika mjini Nakuru Kenya, na kufanikiwa kuwa washindi wa tatu wa michuano hiyo.
wakati wa kushuka daraja hii tumu umewadia...hawajifunzi hata kwa wenzao toto africa
ReplyDelete