SIMBA YAANZISHA GAZETI LAKE
Na George Mganga
Uongozi wa klabu ya Simba umetangaza kuanzisha gazeti lake ambalo litatambulishwa kesho katika tamasha la Simba Day.
Hatua hiyo imekuja mara baada ya uongozi huo kueleza kumekuwa na magazeti baadhi mtaani yamekuwa yakitumia jina la Simba na kujipatia faida ambayo ilipaswa kuwa inaenda klabuni.
Kwa mujibu wa Ofisa Habari wa Simba, Haji Manara, amesema gazeti hilo litakuwa linaitwa SIMBA NGUVU MOJA, litakuwa linatoka mara kila wiki siku ya Jumamosi.
Manara amesema gazeti hilo litakuwa linauzwa siku ya Jumamosi na gharama yake itakuwa kiasi cha shilingi za kitanzania 500 pekee.
Utambulisho wa gazeti hilo utafanyika kesho ambapo Simba itakuwa inakipiga na Asante Kotoko kutoka Ghana ukiwa ni mchezo maalum wa kukitambulisha kikosi cha timu hiyo kuelekea msimu ujao wa Ligi Kuu Bara.
SIMBA nguvu moja? Sikupenda jina hilo kwani hili sio jina bali ni ujumbe. Manara na wingi wa hazina ya maneno Mungu aliekujaalia ulipaswa wewe na viongozi wenzio wa kamati ya ubunifu kutafuta jina lenye asili ya utani zaidi na raha na tayari lililokwishazoeleka. Kwanini Gazeti hilo lisiitwe MNYAMA? na ujumbe unaofuatia ukawa Simba nguvu moja?
ReplyDeleteWakat Yanga wanaanzisha mliponda ama kweli hii ndio tz watu wake vigeu geu
ReplyDeleteAcha magazeti kitu muhimu Radio na TV station
ReplyDelete