August 20, 2018


Majeraha aliyoyapata straika kiwembe wa Simba, Emmanuel Okwi raia wa Uganda katika mchezo wa Ngao ya Jamii dhidi ya Mtibwa, yamemfanya kocha wa timu hiyo, Mbelgiji Patrick Aussems kuingia kiwewe kama ataweza kumtumia straika huyo kwenye mchezo wao wa kwanza wa ligi kuu keshokut­wa Jumatano dhidi ya Tanzania Prisons.

Okwi ambaye ndiye mfungaji bora wa Ligi Kuu Bara msimu uliopita akiwa na mabao 20, alishindwa kuendelea kwenye mchezo wa Ngao ya Jamii kati ya Simba na Mtibwa Sugar uliopigwa juzi Jumamosi kwenye Uwanja wa CCM Kirumba jijini Mwanza, straika huyo alipata majeraha ya enka yaliyosababisha atolewe dakika ya 66 na nafasi yake kupewa John Bocco. Simba walishinda kwa mabao 2-1.

Kocha huyo mwenye mwili mkubwa, amesema kuwa kuumia kwa mshambuliaji wake huyo kumefanya awe na hofu kama ataweza kumtumia kwenye mchezo wao wa kwanza wa ligi kutokana na umuhimu wa nyota huyo kwenye kikosi chake hicho.

“Sijajua Okwi ameumia kwa ukubwa gani baada ya kupata majeraha kwenye mchezo wetu huu dhidi ya Mtibwa Sugar. Un­ajua yeye ni mtu muhimu kwenye timu kutokana na mchango wake ambao amekuwa akiuonyesha kila mara, hivyo ninasikilizia juu ya ripoti ya madaktari kuona ni nini ambacho wao watakisema juu yake.

“Lakini jambo zuri zaidi tumeanza vizuri kwa kuchukua ubingwa na kitu kizuri ni kwamba wachezaji John Bocco na Shomari Kapombe ambao walikuwa nje kutokana na majeraha kwa sasa wamerudi kundini, hivyo inafanya tuwe na timu imara zaidi,” alisema Mbelgiji huyo.

Imebainika kuwa straika huyo anaendelea vizuri baada ya kutolewa kwenye mchezo huo lakini atachunguzwa zaidi baada ya timu hiyo kufika Dar ambapo msafara wao ulitarajiwa kutua jana Jumapili. 

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic