August 22, 2018


Timu ya Simba leo hii inashuka uwanjani kupambana na Tanzania Prisons katika mchezo wake wa kwanza wa Ligi Kuu Bara msimu wa 2018/19 kwenye Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam kuanzia saa 1:00 usiku.

Endapo timu hiyo itaibuka na ushindi katika mechi hiyo, basi itajipatia kitita cha Sh milioni 10 ambazo watapewa wachezaji kwa ajili ya kugawana kama bonasi.

Habari za kuaminika kutoka ndani ya Simba ambazo Championi Jumatano, limezipata zimedai kuwa fedha hizo zitatolewa na uongozi wa timu hiyo ikiwa ni kwa kushirikiana na mwekezaji wake mkuu, Mohammed Dewji ‘Mo’.

“Hatua hiyo ni mwendelezo wa kile kilichokuwa kikifanyika msimu uliopita kwa ajili ya kuwapa motisha wachezaji ili kuhakikisha wanafanya vizuri katika mechi zetu zote.

“Kwa hiyo kila tutakapokuwa tukishinda wachezaji watapewa Sh milioni 10, Sh 5,000,000, zitakuwa zikitolewa na Mo lakini Sh 5,000,000 nyingine zitakuwa zikitolewa na uongozi,” kilisema chanzo hicho.

3 COMMENTS:

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic